-
Jeshi la Sudan ladhibiti maeneo ya Khartoum na kulenga ikulu ya rais
Mar 16, 2025 22:45Duru za habari zimekinukuu chanzo kimoja nchini Sudan kwamba jeshi la nchi hiyo limeshambulia ikulu ya rais mjini Khartoum kwa ndege zisizo na rubani na kudhibiti maeneo ya katika mji mkuu, ambayo baadhi bado yako chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Raila: Nilizuia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Ruto
Mar 16, 2025 09:08Kinara wa Upinzani Raila Odinga amefichua kuwa aliamua kumwokoa Rais William Ruto wakati wa maandamano ya Gen Z ili kuzima mapinduzi ya kijeshi ambayo yalikuwa yamesukwa na yalikuwa yakikaribia tu kutekelezwa.
-
Waislamu na Wakristo Burkina Faso wala futari pamoja kuimarisha umoja
Mar 16, 2025 08:02Mamia ya Waislamu na Wakristo huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, wameshiriki pamoja dhifa ya futari katika medani ya Place De La Nation, kuadhimisha mwaka wa tatu wa utamaduni huo wa kuhamasisha mshikamano wa kijamii, wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na ghasia za itikadi kali.
-
Wahamiaji 194 wa Kiafrika wakamatwa nchini Yemen
Mar 16, 2025 02:33Vikosi vya usalama vya Yemen jana viliwatia mbaroni wahamiaji 194 kutoka eneo la Pembe ya Afrika waliokuwa wakijaribu kuingia nchini humo kinyume cha sheria kupitia mkoa wa Shabwa wa kusini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Ndege za kivita za Marekani na Uingereza zashambulia Yemen, raia 18 wauawa
Mar 15, 2025 23:34Ndege za kivita za Marekani na Uingereza zimeishambulia Yemen kwa ukatili, zikiua raia 18, kufuatia agizo la rais wa Marekani kutumia "nguvu kubwa ya maangamizi" dhidi Yemen baada ya taifa hilo kupiga marufuku meli za Israel kupitia maeneo muhimu ya baharini.
-
Afrika Kusini: Tumesikitishwa na hatua ya Washington ya kumfukuza balozi wetu
Mar 15, 2025 09:35Afrika Kusini imetangaza kuwa uamuzi wa Marekani kumfukuza nchini humo balozi wake, Ebrahim Rasool "unasikitisha", lakini nchi hiyo "bado ina nia ya kujenga uhusiano wa kunufaishana" na Washington.
-
Somalia pia yapinga pendekezo la US kuhusu Wapalestina wa Gaza
Mar 15, 2025 03:40Serikali ya Somali imepinga vikali pendekezo la Marekani la kuwapa makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwenye ardhi ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
MSF yatahadharisha kuhusu kasi kipindupindu Ethiopia; watu 31 wameaga dunia
Mar 14, 2025 22:54Takriban watu 31 wapoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaoenea kwa kasi nchini Ethiopia.
-
AU yatahadharisha kuhusu hali mbaya katika eneo la Tigray nchini Ethiopia
Mar 14, 2025 11:15Umoja wa Afrika (AU) umeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu matukio yanayojiri katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, ambapo mizozo ya kisiasa kati ya pande zinazohasimiana inatishia makubaliano tete ya amani yaliyomaliza vita katika eneo hilo.
-
Wawakilishi wa Sudan na UAE walumbana katika mkutano wa Baraza la Usalama
Mar 14, 2025 09:32Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York uliokuwa ukichunguza hali ya kibinadamu nchini Sudan umeambatana na malumbano na shutuma za pande mbili kati ya wawakilishi wa Sudan na UAE katika Umoja wa Mataifa.