-
Mjumbe wa UN ataka kuimarishwa hadhi ya wanawake nchini Libya
Mar 09, 2025 03:13Hanna Serwaa Tetteh, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ambaye pia ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL ametoa mwito wa kuinuliwa hadhi ya wanawake nchini Libya.
-
Waziri wa Ulinzi wa Sudan: Jeshi limepiga hatua kubwa dhidi ya RSF
Mar 08, 2025 23:08Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Yassin Ibrahim, amesema kuwa jeshi la nchi hiyo limepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Mlipuko wa ugonjwa wa Mpox waukumba mji wa Kabare huku mzozo ukiendelea DRC
Mar 08, 2025 23:07Mji wa Kabare, unaopatikana katika jimbo la Kivu Kusini umeathiriwa na mlipuko mkali wa ugonjwa wa Mpox, ugonjwa ambao kimsingi huambukizwa kupitia mgusano wa karibu wa ngozi hadi ngozi.
-
Ethiopia yaanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya al-Shabab nchini Somalia
Mar 08, 2025 07:50Jeshi la anga la Ethiopia limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab katika Mkoa wa Shabelle ya Kati nchini Somalia. Mashambulizi hayo ya anga yametokea baada ya kutiwa saini mkataba wa usalama kati ya Somalia na Ethiopia mwezi uliopita.
-
Baada ya kutimuliwa na kukabidhi kambi, sasa wanajeshi wa Ufaransa waanza kufungasha virago Senegal
Mar 08, 2025 07:46Baada ya serikali ya Senegal kuwatimua na kuwalazimisha wakabidhi kambi zao, sasa wanajeshi wa mkoloni wa Ulaya yaani Ufaransa, wameanza rasmi kuondoka katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
-
Rais wa Sudan Kusini ataka utulivu baada ya askari 28 kuuawa
Mar 08, 2025 03:31Jenerali wa Jeshi la Sudan Kusini na makumi ya wanajeshi wameuawa baada ya helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa ikijaribu kuwahamisha askari hao kutoka mji wa kaskazini wa Nasir iliposhambuliwa na genge la wanamgambo.
-
Zimbabwe: Tunafanya hima kujiunga na kundi la BRICS
Mar 08, 2025 03:31Zimbabwe inafanya kila liwezekanalo kujiunga na kundi la BRICS, ikilenga kuimarisha uchumi wake na ushirikiano wa kimataifa.
-
Jeshi la Nigeria: Tumeangamiza magaidi 92, tumetia mbaroni 111
Mar 08, 2025 00:56Katika taarifa yake ya karibuni zaidi, jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limeangamiza takriban magaidi 92 na kuwatia mbaroni wengine 111 katika operesheni mbalimbali za wanajeshi wa nchi hiyo kwenye kipindi cha wiki moja iliyopita.
-
Ujangili wakithiri A/Kusini, vifaru 420 wawindwa kinyume cha sheria
Mar 08, 2025 00:56Waziri wa Misitu, Uvuvi na Mazingira wa Afrika Kusini, Dion George, ametoa taarifa rasmi na kusema kuwa vifaru 420 waliuliwa kinyume cha sheria kwa ajili ya pembe zao nchini Afrika Kusini mwaka 2024, ingawa idadi hiyo iko chini ya ile ya mwaka juzi, 2023, ambapo vizuri 499 waliuliwa na majangili kwa ajili ya vipusa.
-
Sudan yaishukuru UNSC kwa kupinga kuundwa serikali nyingine nchini humo
Mar 08, 2025 00:55Serikali ya Jenerali Abdul Fattal al Burhan wa Sudan imetangaza kufurahishwa na taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) ya kupinga juhudi za kuundwa serikali nyingine sambamba na ile inayotawala hivi sasa nchini Sudan.