-
Takriban watu 70 wauawa katika mapigano ya Puntland, Somalia
Feb 06, 2025 23:11Takribani watu 70 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia mapigano ya saa 24 kati ya wapiganaji wa Islamic State na vikosi vya eneo la Somalia la Puntland.
-
UN: Hali ya kibinadamu huko Goma bado ni mbaya licha ya kusimamishwa mapigano
Feb 06, 2025 23:09Hospitali katika mji mkubwa wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Goma, zinatatizika kutibu mamia ya wagonjwa waliojeruhiwa, huku baadhi wakiripoti uhaba wa dawa siku chache baada ya kundi la waasi la M23 kutangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja.
-
Uganda yakanusha kuwatuma wanajeshi wa ziada mashariki ya DRC
Feb 06, 2025 23:08Jeshi la Uganda limekanusha rasmi madai kwamba limepeleka wanajeshi wake Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambapo vikosi vya Congo vinapigana na waasi wa M23.
-
Mahakama ya Kijeshi ya DRC yatoa hati ya kukamatwa Corneille Nangaa
Feb 06, 2025 07:47Mahakama ya Kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Corneille Nangaa, mkuu wa makundi ya waasi wa mashariki mwa nchi hiyo, ikimtuhumu kwa kushindwa kuzuia vitendo vya utesaji chini ya mamlaka yake.
-
UN: Hofu ya magonjwa ya miripuko yatanda katika mji wa Goma unaokaliwa kwa mabavu
Feb 06, 2025 03:24Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Goma wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaokaliwa kwa mabavu, alisema jana Jumatano kuwa mji huo uko katika hali mbaya huku wasaidizi wa masuala ya kibinadamu wakipambana na hatari ya magonjwa ya mripuko.
-
Waasi wa M23 wateka mji mwingine mashariki mwa DRC licha ya kudai kusitisha vita
Feb 06, 2025 03:24Waasi wa M23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano waliuteka mji wa Nyabibwe ulioko mashariki mwa jimbo la Kivu Kusini licha ya kudai kuwa wamesimamisha vita kwa upande mmoja.
-
Jeshi la Sudan lasonga mbele kuelekea katikati ya Khartoum
Feb 05, 2025 23:03Jeshi la Sudan lilitangaza jana, Jumatano, kuwa limepiga hatua kubwa za maendeleo katika mji mkuu, Khartoum, na kudhibiti kitongoji cha Al-Rumaila, makao makuu ya vifaa vya matibabu.
-
Kwa nini Afrika Kusini inataka Marekani iwekewe vikwazo
Feb 05, 2025 23:01Waziri wa Madini na Rasilimali za Petroli wa Afrika Kusini, Gwede Mantashe ametoa wito kwa nchi za Afrika kusimamisha mauzo ya madini kwenda Marekani.
-
"Mapinduzi ya Kiislamu yaliathiri mapambano ya Afrika Kusini dhidi ya apartheid"
Feb 05, 2025 08:48Mwanahabari mkongwe mjini Cape Town, Farid Sayed amesema Mapinduzi ya Kiislamu na kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kulikuwa na athari kubwa kwa mapambano ya Afrika Kusini dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa apartheid.
-
Afrika Kusini yamuonya Trump; Tutasitisha mauzo ya madini kwa Marekani
Feb 04, 2025 23:11Waziri wa Madini na Rasilimali za Petroli wa Afrika Kusini, Gwede Mantashe ametoa wito kwa nchi za Afrika kusimamisha mauzo ya madini kwenda Marekani.