Wazayuni wazidi kutwangana, waziri "aonja joto ya jiwe" + Video
(last modified 2024-09-05T06:04:18+00:00 )
Sep 05, 2024 06:04 UTC
  • Wazayuni wazidi kutwangana, waziri

Wapinzani wa serikali ya Benjamin Netanyahu wamemshambulia waziri wa elimu wa utawala wa Kizayuni huku maandamano ya kupinga udikteta wa Netanyahu na serikali yake ya genge lenye misimamo mikali ya Kizayuni yakizidi kuwa makubwa na makali.

Hayo yameripotiwa na gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth usiku wa kuamkia leo na kuongeza kuwa, waandamanaji wamemshambulia waziri wa elimu wa utawala wa Kizayuni, Yoav Kisch, wakati alipotembelea skuli moja ya msingi katikati mwa ardhi za Palestina ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu waliomshambulia waziri huyo wa Israel walikuwa wamevaa fulana zilizoandikwa tunataka uchaguzi sasa hivi!

 

Gazeti la Yedioth Ahronoth limeongeza kuwa, waandamanaji walimzingira waziri huyo wa elimu wa utawala wa Kizayuni na kuanza kutaja kwa kutumia spika majina ya mateka wa Israel walioko Ukanda wa Ghaza na kuhoji wakisema, kwa nini mateka hao hawajakombolewa? Kwa nini bado wako Ghaza?

Maandamano ya kupinga serikali ya kifashisti ya Netanyahu yamepamba moto kuanzia Jumapili wiki hii baada ya kupatikana miili sita mingine ya mateka wa Palestina kwenye Ukanda wa Ghaza.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa, watatu kati ya mateka hao sita majina yao yalikuwemo kwenye orodha ya watu waliokusudiwa kuachiliwa huru, lakini Benjamin Netanyahu alikwamisha makubaliano hayo na matokeo yake mateka hao wameuawa kwenye mashambulizi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni.