Sep 13, 2023 04:16 UTC
  • Iran yaitandika Angola 4-0 katika Fifa Day

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitandika timu ya soka ya taifa ya Angola mabao 4 kwa sifuri katika mechi ya kirafiki iliyochezwa katika dimba la Azadi mjini Tehran.

Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa ilichezwa jana katika mlolongo wa mechi za kujipima nguvu katika kalenda ya FIFA (FIDA DAY). Vijana wa mkufunzi Amir Ghalenoei jana waliendeleza wimbi la ushindi katika mechi za kujipima nguvu hapo wiki iliyopita waliishinda timu ya Bulgaria bao 1 kwa yai.

Katika mechi ya jana dhidi ya timu ya Kiafrika ya Angola iliyochezwa bila ya kuhudhuriwa na mashabiki, timu ya taifa ya soka ya Iran al-Maarufu Team Melli ilitawala mchezo huo karibu katika sekta zote.

Nyota wa mchezo huo alikuwa mshambuliaji Mehdi Taremi anayechezea Porto ya Ureno. Taremi alipachika mabao mawili huku mabao mengine ya timu ya soka ya taifa ya Iran yakitiwa wavuni na Sadeqi Muharrami na Shahriyry Moghalou.

Tags