Meja Jenerali Salami: Gaza ni kaburi la Marekani na utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i104560-meja_jenerali_salami_gaza_ni_kaburi_la_marekani_na_utawala_wa_kizayuni
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, hii leo Gaza imekuwa uwanja wa kuzikia Marekani na utawala wa Kizayuni, na utawala naoikalii kwa mabavu Quds hauwezi kurejesha nguvu zake zilizopotea.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 09, 2023 09:47 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Gaza ni kaburi la Marekani na utawala wa Kizayuni

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, hii leo Gaza imekuwa uwanja wa kuzikia Marekani na utawala wa Kizayuni, na utawala naoikalii kwa mabavu Quds hauwezi kurejesha nguvu zake zilizopotea.

Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), amesema hayo leo katika hafla ya kufungaKongamano la Kitaifa la Fursa Zinazoibuka na Vitisho vya Baharini na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni unakabiliwa na kushindwa vibaya kusikowezekana kufidika.

Kamanda Salami ameashiria Operesheni ya Kimbunga cha Aqsa, na kusema: "Gaza leo kaburi la kuzikia Marekani na utawala wa Kizayuni.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Utawala wa Kizayuni na nchi nyingine za magharibi zimefikia mahali ambapo zinadhania kwamba, kwa kuua watoto huko Gaza watapata amani na nguvu, lakini wanajua kwamba hawawezi kufikia malengo yao.

Maiti za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Meja Jenerali Salami ameongeza kusema kuwa, Iran iko katika ufuo wa bahari muhimu zaidi duniani na kwamba, asilimia 90 ya biashara ya dunia yakiwemo mafuta na gesi inafanywa kupitia bahari hiyo na kusema: Marekani inatumia fursa ya kuwa katika pwani ya bahari ili kuwa na satwa na na udhibiti kwa nchi zingine, na viongozi wao wanaamini kuwa hawawezi kufikiwa, lakini hii ni sera bandia na ya uwongo.

Akigusia uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kumfanya adui asijaribu kuishambulia katika uga wa bahari na kusema kuwa, mabeberu wa dunia lazima wajue kwamba Iran inaweza kutetea haki na maslahi popote pale duniani.