Amir-Abdollahian: Wakati wa kuendelea jinai za Israel huko Gaza unakaribia mwisho
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i104566-amir_abdollahian_wakati_wa_kuendelea_jinai_za_israel_huko_gaza_unakaribia_mwisho
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muda kuendelea jinai za Israel katikak Ukanda wa Gaza unazidi kuyoyoma haraka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 09, 2023 10:48 UTC
  • Amir-Abdollahian: Wakati wa kuendelea jinai za Israel huko Gaza unakaribia mwisho

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muda kuendelea jinai za Israel katikak Ukanda wa Gaza unazidi kuyoyoma haraka.

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye mitandao ya kijamii Alkhamisi ya leo na kusisitiza kwamba, wakati wa kuendelezwa jinai za Tel Aviv unakaribia kumalizika haraka: Faida pekee ya Netanyahu ni kwamba, aliifanya misingi ya utawala bandia wa Israel kutetereka zaidi na kuuonyesha kwa uwazi uso wa utawala haramu wa Israel katika mauaji ya wanawake na watoto huko Gaza. Abdollahiana amesema kuwa, hapana shaka yoyote kwamba, mustakabali utaluiwa mali ya Wapalestina.

Kuangamizwa Wazayuni zaidi ya 1,500 wakiwemo mamia ya wanajeshi ya utawala huo ghasibu, ni sehemu ndogo ya matunda ya Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ya wanamapambano wa Palestina iliyoanza Oktoba 7.

Jinai za Israel Gaza zimeendelea kulaaniwa kimataifa

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesisitiza haja ya kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu na kutumwa misaada zaidi huko Gaza, akisema kuwa hali ya eneo hilo la Palestina linaloshambuliwa na Israel ni "ya kutisha" na "janga".

Asasai mbalimbali za haki za binadamu za kieneo na kimataifa, zimetangaza kuwa, mauaji makubwa yanayofanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina pamoja na kuwahamisha raia, wanawake na watoto kwa lazima na kinyume cha sheria kuwa ni uhalifu wa kivita.