Abdollahian: Hakuna uwezekano wa Israel kushinda vita vya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i104814-abdollahian_hakuna_uwezekano_wa_israel_kushinda_vita_vya_gaza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa mwito wa kusitishwa mara moja uvamizi na mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, utawala huo wa Kizayuni hauna nafasi na uwezo wa kupata ushindi katika vita hivyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 15, 2023 10:19 UTC
  • Abdollahian: Hakuna uwezekano wa Israel kushinda vita vya Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa mwito wa kusitishwa mara moja uvamizi na mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, utawala huo wa Kizayuni hauna nafasi na uwezo wa kupata ushindi katika vita hivyo.

Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo leo Jumatano mjini Geneva, Uswisi katika mkutano wake na Martin Griffiths, Mkuu wa Operesheni za Dharura na Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kujadili kadhia ya Gaza.

Amir-Abdollahian ameeleza kuwa, "Hakuna uwezekano wowote wa utawala wa Kizayuni kushinda vita, na kitakachofanyika ni kuoingezea tu gharama serikali ya Marekani kama muungaji mkono mkuu Israel."

Amesema Marekani inabeba dhima ya kuendelea uvamizi na hujuma za kinyama dhidi ya Wapalestina wa Gaza, na kwamba kuna haja ya kufanyika jitihada za kusimamisha vita hivyo mara moja.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amebainisha kuwa, kiwango cha misaada ya kibinadamu kilichotumwa na Marekani huko Gaza ni kidogo mno kinyume na wanavyodai Wamarekani na kuongeza kuwa, hatua hiyo ya kupeleka misaada na wakati huo huo inaunga mkono kuendelea vita ni ya kimaonyesho.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran ameongeza kuwa, kupitia mashambulizi mtawalia ya mabomu na mauaji ya halaiki ya watu wa Ukanda wa Gaza, utawala wa Israel umekiuka wazi wazi haki zote za binadamu na sheria za kimataifa.

Zaidi ya Wapalestina elfu 11 na mia mbili wameuawa shahidi hadi sasa tokea Oktoba 7 katika mashambulizi ya maangamizi ya umati yanaotekelezwa na utawala dhalimu wa Israel huko Ukanda wa Gaza, zaidi ya elfu 8 miongoni mwao wakiwa watoto na wanawake. 

Kadhalika Abdollahian ametaja vitendo vya utawala wa Kizayuni katika mashambulizi yake ya kikatili ya kama kulenga shule, hospitali, ambulensi na vituo vya kutoa huduma za afya huko Ukanda wa Gaza kuwa ni jinai ya kivita.

Kwa upande wake, Martin Griffiths, Mkuu wa Operesheni za Dharura na Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa mbali na kusema kuwa ameridhishwa na mkutano wake na Abdollahian, ametoa mwito wa kuongezwa jitihada za kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza. Aidha amesema kuwa amesikitishwa na hali ya hospitali ya al-Shifaa huko Gaza, iliyoshambuliwa na jeshi la Israel.