Apr 06, 2024 06:57 UTC
  • Rais wa Iran: Walimwengu watajionea kuangamia kwa utawala wa Kizayuni

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu maalumu za kuwashukuru wananchi walio macho na wenye kujali thamani ya mambo wa Iran kwa ushiriki wao mkubwa katika matembezi ya Siku ya Quds Duniani na kusema: Walimwengu watajionea kuangamia kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa Shirika Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, katika salamu zake, Rais Ebrahim Raisi, amepongeza kushiriki kwa ukakamavu wananchi walio macho na wenye kujali thamani ya mambo wa Iran na akasema, mahudhurio hayo yanatuma ujumbe wa wazi kwa Uistikbari duniani kwamba, mwisho wa dhulma na uporaji, uchokozi na mauaji huwa ni kushindwa tu.

 
Seyyid Raisi ameongeza kuwa: leo kwa baraka za ghera na ushujaa wa Wapalestina, imewadhihirikia watu wote kwamba kasri bandia la Uzayuni ni dhaifu zaidi kuliko utando wa buibui.
 
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, ni hakika kabisa, kwamba harakati hiyo ya umma na ya ulimwengu mzima itazaa matunda na walimwengu watakuja kujionea kuthibiti kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu na kuangamia kwa utawala wa Kizayuni.

Jana, Ijumaa, Aprili 5, 2024 sawa na Ramadhani 25, 1445, ilikuwa Siku ya Kimataifa ya Quds.

 
Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imepewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa ubunifu wa Imam Khomeini (RA), mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
 
Baada ya kutangazwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, Umma wa Kiislamu unaitazama kadhia ya Palestina kuwa ni suala la dharura na lenye ulazima, katika kuyaunga mkono mataifa yanayodhulumiwa na yanayonyongeshwa.

Matembezi ya Siku ya Quds Duniani jana Ijumaa yalifanyika katika miji na vijiji zaidi ya elfu mbili nchini Iran kwa kuhudhuriwa na wananchi wakakamavu wa Iran.../

 

 

Tags