Jun 15, 2024 12:04 UTC
  • Ayatullah Khamenei: Fanyeni hima ili ushiriki katika uchaguzi uongezeke

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ameashiria umuhimu mkubwa wa uchaguzi na kubainisha juu ya udharura wa kufanyika juhudi za kuwafanya watu washiriki kwa wiingi katika uchaguzi.

Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo alipokutana na kundi la wenye vipaji na vijana wa Kiirani waliotwaa medali katika mashindano ya kielimu na kuwaambia kwamba, wanapaswa kujaribu kadiri wawezavyo kuongeza ushiriki katika uchaguzi na juhudi hizo ziwe katika mazingira ya kiuwanafunzi, ya kikazi au ya kifamilia.

Kiongozi Muadhamu ameashiria vigezo vya kuchagua Rais ajaye na kuwataka watu wazingatie suala la uwezo katika vigezo mapinduzi.

Kuhusiana na suala la elimu, Ayatullah Khamenei amesema: Nchi yetu ilianza harakati za kisayansi, hatua ya kisayansi zaidi ya miaka 20 iiliyopita. Kwa kweli, kazi ya kisayansi imefanywa tangu miongo kadhaa lakini tangu mwaka 2000, msukumo wa umma ulifanyika katika mazingira ya wahadhiri na katika mazingira ya wanafunzi. Kiongozi Muadhamu amesema, harakati hiyo ya imekuwa kubwa kiasi kwamba, takwimu za kimataifa zilionyesha kwamba, tunapiga hatua mara kadhaa ya wastani wa dunia katika kiwango cha maendeleo ya kisayansi.

Pamoja na mafanikio ya Iran katika nyuga mbalimbali za kielimu, Kiongozi Muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia kuongezwa juhudi zaidi.

Amesema, katika miaka hii miwili au mitatu ya hivi karibuni kumefanyika harakati kubwa ya kielimu, lakini harakati hii haitoshi, kwani sisi tunahitaji vuguvugu la kielimu na akawahutubu vijana waliotwaa medani za kielimu kwa kuwaambia, nyinyi mnaweza kufanya kazi athirifu katika uga huu.