Vyombo vya habari vya nje 150 kuripoti uchaguzi wa Rais wa Iran
(last modified Tue, 25 Jun 2024 07:45:55 GMT )
Jun 25, 2024 07:45 UTC
  • Vyombo vya habari vya nje 150 kuripoti uchaguzi wa Rais wa Iran

Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa vyombo vya habari vya nje 150 kutoka nchi 31 vitaripoti zoezi la uchaguzi wa rais wa Iran utaofanyika Ijumaa ijayo Juni 28.

Alireza Shirovi, Mkurugenzi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Kigeni wa Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa: Zaidi ya waandishi wa habari 500 kutoka vyombo vya habari vya nje 150 vyenye makazi yake hapa nchini na kinyume chake kutoka nchi 31 wataripoti  uchaguzi wa 14 wa Rais wa Iran. 

Wagombea katiak uchaguzi wa Rais wa Iran 

Shirovi ameashiria mapokezi makubwa ya vyombo vya habari vya nje katika duru kadhaa zilizopita za uchaguzi wa Rais wa Iran na kuongeza kuwa: Kulingana na maombi yaliyopokelewa hadi sasa, vyombo vya habari kutoka Austria, Uhispania, Australia, Marekani, Uingereza, Italia, Azerbaijan, Ujerumani, Bahrain, Pakistan, Uturuki, Algeria, China, Denmark, Russia, Zimbabwe, Japan, Syria, Sweden, Iraq, Oman, Ufaransa, Palestina, Kyrgyzstan, Qatar, Korea Kusini, Korea Kaskazini, Colombia, Kuwait, Lebanon na Yemen vimethibitishwa kuwa vitarusha matangazo wakati wa duru ya 14 ya uchaguzi wa Rais wiki hii.

Uchaguzi wa 14 wa Rais wa Iran utafanyika Ijumaa, Juni 28, 2024.