Dakta Velayati: Iran inasisitiza juu ya kupambana na utumiaji mabavu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i11515-dakta_velayati_iran_inasisitiza_juu_ya_kupambana_na_utumiaji_mabavu
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratijia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kuweko ushirikiano zaidi baina ya nchi za Bara Asia kwa ajili ya kufikia malengo ya ustawi na vita dhidi ya utumiaji mabavu na vitendo vya uchupaji mipaka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2016 23:51 UTC
  • Dakta Velayati: Iran inasisitiza juu ya kupambana na utumiaji mabavu

Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratijia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kuweko ushirikiano zaidi baina ya nchi za Bara Asia kwa ajili ya kufikia malengo ya ustawi na vita dhidi ya utumiaji mabavu na vitendo vya uchupaji mipaka.

Dakta Ali Akbar Velayati aliyasema hayo huko nchini Singapore jana katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wahajiri wa Kiasia na kubainisha kwamba, umasikini, kubaki nyuma kimaendeleo, kutokuweko usalama, mitazamo ya upande mmoja na uchupaji mipaka ni miongoni mwa matatizo yanayoikabili jamii ya mwanadamu hii leo.

Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiistratijia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema bayana kwamba, matatizo ya pamoja ya nchi za Asia ni jambo linalotoa udharura wa kuweko mitazamo ya pamoja ya kieneo kwa shabaha ya kupatikana ustawi wa kudumu na kufikia malengo ya kupambana na vitendo vya uchupaji mipaka na vita dhidi ya ugaidi.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesisitiza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa ikisisitiza juu ya kupambana na vitendo vya utumiaji mabavu na misimamo ya kuchupa mipaka.

Amesema, kutokana na uwezo ilionao Iran wa kiuchumi na kiusalama inaweza kuandaa fursa mwafaka kwa ajili ya kushirikiana na nchi za Asia katika uwanja huo.