Mazoezi ya pamoja ya majeshi ya majini ya nchi za Bahari ya Hindi yaanza Iran
(last modified 2024-10-19T11:43:51+00:00 )
Oct 19, 2024 11:43 UTC
  • Mazoezi ya pamoja ya majeshi ya majini ya nchi za Bahari ya Hindi yaanza Iran

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya  Majeshi ya Majini ya nchi za Kandokando ya Bahari ya Hindi (IONS) ), "IMEX 2024," yameanza katika eneo la maji ya Iran katika Ghuba ya Uajemi kwa kuvishirikisha vitengo mbalimbali kutoka nchi kadhaa wanachama na waangalizi.

Admeri Mostafa Tajeddini, Msemaji wa mazoezi ya pamoja ya  Majini ya IMEX 2024 amesema luteka hiyo ambayo imeandaliwa na Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kitengo cha majini cha Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Shirika la Bandari na Bahari, limeanza katika Mkoa wa Kwanza wa Wanamaji wa Jeshi la Wanamaji la Irani katika mji wa bandari wa Bandar Abbas siku ya Jumamosi.

Ameongeza kuwa nchi kadhaa za kigeni kama Bangladesh, India, Oman, Pakistan, Qatar, Russia, Saudi Arabia na Thailand zimetuma vikosi vyao vya majini kushiriki katika mazoezi hayo ya baharini pamoja na wenzao wa Iran.

Tajeddini amebainisha kuwa zoezi la pamoja la IONS IMEX 2024 la wanamaji litajumuisha mikutano na warsha maalum ili kubadilishana uzoefu baina ya  vikosi vinavyoshirikiA .mesema kuwa vitengo vinavyoshiriki katika mazoezi ya pamoja ya majini vitafanya mazoezi mbalimbali kama vile udhibiti wa moto, shughuli za utafutaji na uokoaji pamoja na mbinu za kurejesha na kusafisha mafuta.

Admeri Mostafa Tajeddini, Msemaji wa mazoezi ya pamoja ya  Majini ya IMEX 2024

Tajeddini amesema Luteka ya  wanamaji ya IMEX 2024 inafanyika chini ya kauli mbiu ya "Pamoja kwa Bahari ya Hindi iliyo Salama na Thabiti" na imebeba ujumbe wa amani, urafiki, na ushiriki wa pamoja.

Kongamanlo la Majeshi ya Majini ya nchi za Kandokando ya Bahari ya Hindi (IONS)  lina nchi wanachama 24 katika Bahari ya Hindi, na hufanya mazoezo ya baharini na mikutano kila baaya ya miaka miwili.

Nchi za Afrika zikiwemo Kenya, Tanzania, Mauritius, Msumbiji, Afrika Kusini na Ushelisheli pia ni wanachama wa Kongamano la Wanamaji wa Bahari ya Hindi.

 

Tags