Iran yasambaza vifurushi vya chakula na maji kwa wakaazi wa Gaza
Shirika la Hilali Nyekundu la Iran limesambaza vifurushi vya chakula na maji katika Ukanda wa Gaza ili kusaidia mahitaji ya dharura ya wakaazi wa Ukanda huo ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa mahitaji ya dharura kama chakula na maji.
Hatua hii inafanywa ili kuwaunga mkono wananchi wa Ukanda wa Gaza, ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na maji, na kudhihirisha mshikamano na juhudi za kibinadamu za Iran katika kukabiliana na janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Hatua hii ya Hilali Nyekundu ya Iran sio tu inajibu mahitaji ya dharura ya watu wa Ukanda wa Gaza, lakini pia inatambuliwa kama ishara ya mshikamano na juhudi za kibinadamu katika kukabiliana na migogoro ya kibinadamu. Hatua hii ya Iran pia inaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuuigwa na nchi nyingine kwa ajili ya kukabiliana na migogoro kama hiyo.
Katika siku hizi ambazo utawala wa Kizayuni kwa ukatili usio na kifani, umegeuza barabara za Gaza kuwa machinjio na watu wasio na ulinzi wa ardhi hii wanaangamizwa chini ya mashambulizi ya mabomu, vizuizi vya chakula, na mauaji ya kimbari yaliyolengwa, Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran imeweza kufungua dirisha la matumaini kwa kuvunja ukuta wa vikwazo na kimya cha kimataifa.
Misaada ya kibinadamu ya Iran ikiwa ni pamoja na kupika na kusambaza chakula cha moto miongoni mwa wakimbizi wa Kipalestina, imefika Gaza kwa uratibu na kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa, ili sauti ya huruma na ubinadamu iweze kusikika katika moyo wa maafa hayo ya kibinadamu.