Araqchi: Iran iko macho na imejiandaa dhidi ya uingialiaji wowote wa kigeni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135550-araqchi_iran_iko_macho_na_imejiandaa_dhidi_ya_uingialiaji_wowote_wa_kigeni
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na China wamesisitiza umuhimu wa kudumisha utulivu, kuheshimu uhuru wa nchi, na nafasi muhimu ya kidiplomasia katika kuzuia kuongezeka mizozo na mivutano.
(last modified 2026-01-16T11:14:38+00:00 )
Jan 16, 2026 11:14 UTC
  • Araqchi: Iran iko macho na imejiandaa dhidi ya uingialiaji wowote wa kigeni
    Araqchi: Iran iko macho na imejiandaa dhidi ya uingialiaji wowote wa kigeni

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na China wamesisitiza umuhimu wa kudumisha utulivu, kuheshimu uhuru wa nchi, na nafasi muhimu ya kidiplomasia katika kuzuia kuongezeka mizozo na mivutano.

Katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyyed Abbas Araghchi, alitoa ufafanuzi kuhusu hali ya ndani ya Iran na kusema kwamba, sehemu kubwa ya machafuko ya hivi karibuni ina mizizi yake katika uchochezi na uingiliaji kati wa wahusika wa kigeni, na kwamba hatua zilizochukuliwa zimeanza mchakato wa kurejesha utulivu nchini.

Araghchi amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko macho na imejiandaa dhidi ya uingiliaji wowote wa wageni katika masuala yake ya ndani, lakini wakati huo huo inaacha wazi mlango wa mazungumzo na ushirikiano mzuri na nchi rafiki na Jirani.

Sayyid Abbas Araghchi amezungumzia pia nafasi ya China katika matukio ya kikanda na kimataifa na kutoa wito kwa Beijing kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kuimarisha amani na utulivu katika eneo hili.

Kwa upande wake Wang Yi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China amesema katika mazungumzo yake na Abbas Aarghchi kwamba, Beijing imekuwa ikifuata kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, na kutangaza kwamba nchi yake inapinga sera za mashinikizo, vitisho, na maamuzi ya utwishaji mambo upande mmoja kwa wengine, na inaunga mkono utatuzi wa mizozo kupitia njia za amani.