Araqchi: Yoyote anayeendeleza vita atakwama kwenye kinamasi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137198-araqchi_yoyote_anayeendeleza_vita_atakwama_kwenye_kinamasi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mahojiano yake na mwandishi habari Tom Llamas wa televisheni ya NBC kwamba: Serikali ya Marekani inahusika kikamilifu na umwagaji damu unaoshuhudiwa hivi sasa.
(last modified 2026-03-06T09:20:05+00:00 )
Mar 06, 2026 09:20 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mahojiano yake na mwandishi habari Tom Llamas wa televisheni ya NBC kwamba: Serikali ya Marekani inahusika kikamilifu na umwagaji damu unaoshuhudiwa hivi sasa.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Sayyid Abbas Araqchi ameeleza kuwa vikosi imara vya ulinzi vya Iran ambavyo vimejiandaa kwa muda mrefu kwa ajili ya vita hivi vitamuonyesha yoyote anayetaka kuendeleza vita kuwa amejitumbukiza mwenyewe kwenye kinamasi.

Ameongeza kuwa: Tumefanya mazungumzo mara mbili na serikali ya Marekani na katika mara zote mbili tumeshambuliwa tukiwa katikati ya mazungumzo na kuongeza kuwa Serikali ya Washington inahusika kikamilifu na umwagaji damu unaoshuhudiwa.

Katika mahojiano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Iran ina hakika kwamba itakabiliana na mashambulizi ya nchi kavu ya Marekani dhidi yake. "Tunawasubiri," amesema Sayyid Abbas Araqchi katika mahojiano hayo maalumu na televisheni ya NBC ya Marekani.