Kamanda Talaei-Nik: Trump hana chaguo ila kukubali haki ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138574-kamanda_talaei_nik_trump_hana_chaguo_ila_kukubali_haki_ya_iran
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran amesema: "Kushindwa adui kufungamana na matakwa halali ya taifa la Iran kutasababisha gharama kubwa na kushindwa zaidi adui Mzayuni na Marekani."
(last modified 2026-05-23T12:32:33+00:00 )
May 23, 2026 12:29 UTC
  • Kamanda Talaei-Nik, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran
    Kamanda Talaei-Nik, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran amesema: "Kushindwa adui kufungamana na matakwa halali ya taifa la Iran kutasababisha gharama kubwa na kushindwa zaidi adui Mzayuni na Marekani."

Brigedia Jenerali Reza Talaei-Nik  ameashiria kutumbukia Trump kwenye kinamasi cha vita na vita na Iran na kusema: Trump hana budi ila kukubali matakwa ya wananchi wa Iran na haki za nchi yetu."

Ameongeza kuwa: "Katika medani zote za vita na diplomasia, njia pekee ya kujiondoa adui Marekani na utawala wa Kizayuni katika vita vya tatu vya kulazimisha ni kuwakidhia wananchi wa Iran matakwa yao.

KamandaTalaei -Nik amesema kuwa: "Kushindwa adui kutekeleza matakwa halali ya wananchi wa Iran kutasababisha gharama kubwa zaidi na kushindwa mtawalia Trump na adui Mzayuni."

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran amesema: Trump anapasa kukubali mapendekezo ya Iran na kutilia maanani kuzuia uharibifu na gharama kubwa za kuendeleza vita kwa ajili ya watu wa Marekani na jamii ya kimataifa.

"Kutojali na kupuuza Trump maslahi ya Marekani, kushirikiana kwake na utawala wa kizayuni ya tabia yake ya kiburi vyote hivyo vitaizamisha zaidi Marekani kwenye kinamasi cha vita.