Ayatullah Amoli Larijani: Iran haitishiki na vitisho vya aina yoyote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i22399-ayatullah_amoli_larijani_iran_haitishiki_na_vitisho_vya_aina_yoyote
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, vitisho havina athari yoyote ile kwa moyo wa kijihadi wa taifa la Iran.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 30, 2016 04:49 UTC
  • Ayatullah Amoli Larijani: Iran haitishiki na vitisho vya aina yoyote

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, vitisho havina athari yoyote ile kwa moyo wa kijihadi wa taifa la Iran.

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani amebainisha kwamba, madhali moyo wa kupigana jihadi na kuwapenda Ahlul-Baiti AS ungali upo katika nyoyo za wananchi wa Iran, hilo ni jambo lenye thamani kubwa na ni ngao kwa taifa hili na kwa msingi huo hakuna hatari yoyote ile inayoweza kutishia mfumo na wananchi wa taifa hili la Kiislamu.

Ayatullah Amoli Larijani amebainisha kwamba, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nguvu mno katika eneo la Mashariki ya Kati kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imegeuka kuwa kimbilio la amani na usalama kwa nchi madhulumu ulimwenguni.

Ayatullah Amoli Larijani, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran

Ayatullah Larijani aidha amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawasaidia Waislamu wote na wanaodhulumiwa, majirani na walimwengu kwa mujibu wa misingi na mafundisho ya Kiislamu na kwa mujibu wa vigezo vya kimaadili.

Amesema kuwa, kuweko Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi za Iraq na Syria kumefanyika kwa maombi ya serikali husika na wananchi wa nchi hizo na kwamba, mji wa Halab umekombolewa kwa baraka za uwepo wenye baraka wa kupigana jihadi Wairani bega kwa bega na ndugu zao Wasyria.