Qassemi: Watawala wa Marekani wapate funzo kutoka matukio yaliyopita
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31814-qassemi_watawala_wa_marekani_wapate_funzo_kutoka_matukio_yaliyopita
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Watawala wapya wa Marekani wapate funzo kutoka matukio yaliyopita na kwa msingi huo wakizungumza na taifa la Iran watumie lugha ya heshima."
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Jul 15, 2017 09:23 UTC
  • Qassemi: Watawala wa Marekani wapate funzo kutoka matukio yaliyopita

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Watawala wapya wa Marekani wapate funzo kutoka matukio yaliyopita na kwa msingi huo wakizungumza na taifa la Iran watumie lugha ya heshima."

Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo leo Jumamosi katika kujibu matamshi yasiyo na busara ya rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran akiwa safarini nchini Ufaransa. Qassemi ameongeza kuwa: "Washauri wa rais wa Marekani wanafuata mkondo uliochafuka wa miaka iliyopita na hivi sasa hawana habari na matukio ya Iran eneo na dunia nzima."

Siku ya Alhamisi, Rais wa Marekani akiwa katika kikao cha waandishi habari alipokuwa ameandamana na mwenyeji wake Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kwa mara nyingine alitoa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kudai eti Jamhuri ya Kiislamu ni tishio kuu kwa nchi za Kiarabu. Aidha alidai kuwa eti Marekani inajitahidi kuleta uthabiti duniani.

Rais Trump wa Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameishauri serikali mpya ya Marekani izingatie nafasi chanya ya Iran katika kuleta uthabiti katika eneo na dunia. Amewataka watawala wa Washington wafahamu kuwa migogoro iliyopo inatokana na maamuzi yenye utata, sera haribufu na za kujitanua za Markeani yenyewe na waitifaki wake wavamizi na maghasibu katika eneo.