Meja Jenerali Jaafari: Iran ni nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i34935-meja_jenerali_jaafari_iran_ni_nguvu_kubwa_katika_mashariki_ya_kati
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, SEPAH amesema kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu imegeuka na kuwa nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati na kwamba madola makubwa duniani yanakiri ukweli na uhakika huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 27, 2017 22:59 UTC
  • Meja Jenerali Jaafari: Iran ni nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, SEPAH amesema kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu imegeuka na kuwa nguvu kubwa katika Mashariki ya Kati na kwamba madola makubwa duniani yanakiri ukweli na uhakika huu.

Meja Jenerali Muhammad Ali Jaafari amesema hayo katika mji wa Khozestan wa kusini magharibi mwa Iran na kuongeza kuwa, muqawama na kusimama kidete ni somo kubwa kabisa ambalo lilitolewa na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kupatiwa walimwengu.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, SEPAH amebainisha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni kwa baraka za damu za mashahidi, walimwengu wanashuhudia bayana ushindi wa wanyonge mkabala na ubeberu katika nchi za Mashariki ya Kati na kwamba, haya ni matunda makubwa ya taifa la Iran katika kipindi cha kujihami kutakatifu ambayo walimwengu wamepatiwa.

Meja Jenerali Muhammad Ali Jaafari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, SEPAH

Meja Jenerali Muhammad Ali Jaafari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, SEPAH sambamba na kubainisha kwamba, vijana wanamapinduzi na waumini katika Mashariki ya Kati kwa kusimama kwao kidete wamepata mafanikio makubwa ameongeza kuwa, utamaduni wa muqawama na kusimama kidete baina ya vijana waumini wa Kiirani na wasiokuwa wa Kiirani umekita mizizi na hivi sasa vijana hao wako katika medani ya vita nchini Syria wakipambana na ukafiri na uistikbari.

Kamanda Jaafari ameashiria wasiwasi na kihoro cha utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na ushindi wa muqawama katika Mashariki ya Kati na kusema kuwa, utawala huo umekiri uwepo wenye ushindi wa Iran katika mipaka ya Syria na Iraq na katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh.