Trump azidi kupingwa, Wamarekani wengi waunga mkono JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i35619-trump_azidi_kupingwa_wamarekani_wengi_waunga_mkono_jcpoa
Huku misimamo ya serikali ya Marekani iliyo dhidi ya Iran ikizidi kuchachamaa, uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni kabisa unaonesha kuwa, Wamarekani walio wengi hawakubaliani na misimamo ya Donald Trump na wanaunga mkono makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 14, 2017 00:48 UTC
  • Trump azidi kupingwa, Wamarekani wengi waunga mkono JCPOA

Huku misimamo ya serikali ya Marekani iliyo dhidi ya Iran ikizidi kuchachamaa, uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni kabisa unaonesha kuwa, Wamarekani walio wengi hawakubaliani na misimamo ya Donald Trump na wanaunga mkono makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1.

Shirika la habari la IRIB limetangaza habari hiyo na kusema kuwa, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya YouGov  yanaonesha kuwa asilimia 56 ya Wamarekani wanaunga mkono JCPOA na ni asilimia 19 tu ndio wanaoyapinga makubaliano hayo ya nyuklia.

Matokeo ya uchunguzi huo yanaonesha pia kwamba, asilimia 68 ya wanachama wa chama cha Democrat wanaunga mkono JCPOA na asilimia 22 kati yao wamesema hawana maoni yoyote kuhusu suala hilo. Asilimia 51 ya wanachama wa Republican nao wanaunga mkono makubaliano hayo.

Donald Trump, rais wa Marekani mwenye chuki za kidini na kikabila

 

Makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yaliyotiwa saini kati ya Iran na kundi la 5+1 linaloundwa na nchi za Uingereza, Ufaransa, Russia, China, Marekani na Ujerumani, yalianza kutekelezwa mwezi Januari 2016, hata hivyo muda wote huu Marekani imekuwa ikifanya njama za kuyavuruga.

Msimamo hasi wa rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya makubaliano hayo umekumbwa na upinzani mkubwa katika kona mbalimbali za dunia, bali hata viongozi wengi wa Marekani nao wanampinga Trump katika jambo hilo.