Mar 23, 2016 02:22 UTC
  • Zarif alaani mashambulizi ya kigaidi ya Ubelgiji

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzo kwa simu na mwenzake wa Ubelgiji akilaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea jana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Brussels.

Katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Didier Reynders, Muhammad Javad Zarif ametoa salamu za rambirambi kwa taifa la Ubelgiji na familia za wahanga wa mashambulizi hayo. Dakta Zarif amesema ugaidi na misimamo mikali ni tatizo la dunia nzima na mapambano yake yanahitajia hatua za kimataifa.

Mashambulizi yaliyotokea jana Jumanne katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels yameua watu wasiopungua 36 na kujeruhi wengine 198.

Awali pia Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alilaani vikali mashambulizi ya Brussels katika ukurasa wake wa Twitter na kutoa mkono wa pole kwa serikali na taifa la Ubelgiji hususan familia zilizopoteza wapendwa wao katika mashambulizi hayo.

Tags