Zarif: Iran ndiyo nchi yenye amani zaidi katika Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i40479-zarif_iran_ndiyo_nchi_yenye_amani_zaidi_katika_mashariki_ya_kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ndiyo nchi yenye amani zaidi na yenye nguvu kubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati licha ya mashinikizo yote ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 17, 2018 02:54 UTC
  • Zarif: Iran ndiyo nchi yenye amani zaidi katika Mashariki ya Kati

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ndiyo nchi yenye amani zaidi na yenye nguvu kubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati licha ya mashinikizo yote ya kimataifa.

Muhammad Javad Zarif ambaye anafuatana na Rais Hassan Rouhani katika safari yake nchini India amewaambia Wairani wanaoishi nchini humo kwamba, katika miaka iliyopita nchi zote wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ziliweka vikwazo na kuchukua maamuzi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba katika kipindi cha miaka 40 iliyopita Iran imekuwa chini ya vikwazo vikali zaidi na mashinikizo ya nchi kubwa lakini imeweza kupata maendeleo makubwa kwa kutegemea nguvu ya wananchi wake. 

Muhammad Javad Zarif amesema kuwa, hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa nguzo muhimu na yenye taathira katika masuala ya kimataifa kutokana na mchango wa watu wake. Ameongeza kuwa maendeleo yote ya kisayansi, kiuchumi na mafanikio ya Iran katika nyanja za kimataifa ni matokeo ya kujitolea kwa wananchi na kwamba kwa sababu hiyo viongozi wa nchi wanapaswa kufanya jitihada kubwa zaidi katika kuwahudumia raia. 

Muhammad Javad Zarif

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yuko India kwa safari rasmi ya siku tatu na anaongoza ujumbe wa ngazi ya juu unaojumuisha mawaziri kadhaa na wanaharakati wa masuala ya uchumi. Hii leo Jumamosi Rais Rouhani anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa India na maafisa wengine kadhaa wa ngazi za juu na kushiriki katika kikao cha kiuchumi cha pande hizo mbili.