May 01, 2018 17:32 UTC

Mashindano ya 35 ya Kimataifa ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Iran yalimalizika Jumatano 15 Aprili hii huku kukitolewa wito wa Umoja na kushikamana na Qur'ani Tukufu.

Katika taarifa ya mwisho iliyotolewa baada ya kumalizika mashindano hayo washiriki waliashiria njama za madola ya kiistikbari na utawala wa Kizayuni katika kuibua mifarakano katika umma wa Kiislamu na kusema: "Kushikamana na Qur'ani Tukufu na kutekeleza mafundisho yake ndio njia pekee ya kuuokoa Umma wa Kiislamu."

Mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani yalifanyika kwa muda wa wiki moja kwa kaulimbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja" sambamba na kuanza sherehe za mwezi huu mtukufu wa Shaaban na yaliwajumuisha wasomaji na waliohifadhi Qur'ani  258 kutoka nchi 84. Kulikuwa na washiriki pia kutoka nchi za Afrika Mashariki na tulipata fursa ya kuzungumza na moja kati ya washiriki

Tags