Larijani: Ni upuuzi kufanya mazungumo na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46370-larijani_ni_upuuzi_kufanya_mazungumo_na_marekani
Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema hakuna umuhimu na maana yoyote kufanya mazungumzo na Marekani, baada ya Washington kujiondoa kiwepesi kwenye mapatano ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2018 21:44 UTC
  • Larijani: Ni upuuzi kufanya mazungumo na Marekani

Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema hakuna umuhimu na maana yoyote kufanya mazungumzo na Marekani, baada ya Washington kujiondoa kiwepesi kwenye mapatano ya kimataifa.

Huku akiashiria baadhi ya mapendekezo yanayotolewa ya kufanya mazungumzo na Marekani, Ali Larijani amesema Iran haiwezi kupoteza muda wake kufanya mazungumzo na nchi hiyo ambayo haiheshimu mapatano ya kimataifa.

Spika wa Bunge la Iran aliyasema hayo jana Jumanne katika mkutano wa Idara ya Mahakama hapa Tehran na kuongeza kuwa, Iran ilifikia makubaliano ya nyukia ya JCPOA kati yake, Marekani na nchi za Ulaya, lakini dunia imeshuhudia mkiukaji wa makubaliano hayo ni nani.

Vikwazo vya US dhidi ya Iran

Amesema "Baadhi ya watu wanatoa mwito wa Iran kufanya mazungumzo na Marekani, dola ambalo limejiondoa kwenye Mkataba wa Tabianchi wa Paris, makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kadhalika, (Donald Trump) hana ukomavu wa kisiasa."

Sanjari na kuashirika njama za maadui za kutaka kuvuruga usalama wa taifa hili, Ali Larijani amebainisha kuwa, kila mmoja anapaswa kuelewa fika kwamba, lengo la kuasisiwa magenge ya kigaidi na Marekani na waitifaki wake, ni kulihujumu taifa la Iran, lakini nchi hii imekuwa ikizima njama hizo za maadui.