Zarif: Silaha zinazouzwa nje na Marekani zinavuruga amani ya dunia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46884-zarif_silaha_zinazouzwa_nje_na_marekani_zinavuruga_amani_ya_dunia
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekosoa gharama kubwa ya masuala ya kijeshi inayotumiwa na Marekani akisema suala hilo linavuruga amani na usalama wa dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 19, 2018 11:08 UTC
  • Zarif: Silaha zinazouzwa nje na Marekani zinavuruga amani ya dunia

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekosoa gharama kubwa ya masuala ya kijeshi inayotumiwa na Marekani akisema suala hilo linavuruga amani na usalama wa dunia.

Muhammad Javad Zarif amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: Marekani imevuruga amani ya dunia kutokana na uuzaji wa silaha na inaharibu bure fedha nyingi katika ununuzi na utengenezaji silaha ambazo zingeweza kutumiwa kwa ajili ya kuboresha mustakbali wa dunia.

Waziri wa Mashauri wa Kigeni wa Iran amesema kuwa silaha za Marekani hazikuweza hata kulinda usalama na amani ya raia wa nchi hiyo yenyewe na kuongeza kuwa: Bajeti kubwa ya kijeshi ya Marekani ambayo ni sawa na asilimia 35 ya bajeti ya dunia nzima ya maswala ya kijeshi haikuweza kuzuia mauaji na kujeruhiwa zaidi ya raia elfu 9 wa nchi hiyo katika mashambulizi ya Septemba 11, 2001 yaliyofanywa na raia 15 wa Saudi Arabia. 

Mashambulizi ya 11 Septemba, 2001 yalifanywa na Wasaudia 15

Katika mashambulizi hayo karibu watu elfu tatu waliuawa na wengine zaidi ya elfu 6 walijeruhiwa. Maafisa wa serikali ya Marekani walisema kuwa wanachama wa kundi la al Qaida ndio waliotekeleza mashambulizi hayo. 

Watu 15 kati ya 19 walioshiriki kufanya mashambulizi hayo ya Septemba 11 nchini Marekani walikuwa raia wa Saudi Arabia.