Ndoto za Trump za kuuondoa madarakani utawala wa Kiislamu nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i48753-ndoto_za_trump_za_kuuondoa_madarakani_utawala_wa_kiislamu_nchini_iran
Kamanda wa Jeshi la Wazlini wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) amesema kuwa: Rais Donald Trump wa Marekani anakosea kwa kudhani kuwa Iran imedhoofika baada ya yeye kushika madaraka ya nchi huko Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 12, 2018 23:13 UTC
  • Ndoto za Trump za kuuondoa madarakani utawala wa Kiislamu nchini Iran

Kamanda wa Jeshi la Wazlini wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) amesema kuwa: Rais Donald Trump wa Marekani anakosea kwa kudhani kuwa Iran imedhoofika baada ya yeye kushika madaraka ya nchi huko Marekani.

Brigedia Jenerali Muhammad Ali Ja'fari amesem: Kama Iran, kwa mujibu wa matamshi ya Trump mwenyewe, ilikuwa na uwezo wa kukabiliana na adui kwa ajili ya kujilinda katika kipindi cha dakika 12 tu kabla ya yeye kushika madaraka, basi anapaswa kuelewa kwamba, kipindi hicho sasa kumepungua zaidi. 

Tangu aliposhika hatamu za kuongoza Marekani, Donald Trump amedumisha sera za uhasama mkubwa za Washington dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa tofauti kwamba, mara hii kiongozi huyo amekuwa na ndoto na njozi nyingi kuhusiana na uwezo na hakika ya Jamhuri ya Kiislamu. Trump anatumia majukwaa yote ya ndani na nje ya nchi yake akifanya jitihada za kutaka kuonesha kuwa sera zake hizo zimefanikiwa. Hata hivyo jumbe zote za Trump katika mtandao w akijamii wa Twitter zinaonesha kuwa, kiongozi huyo mwanagenzi katika masuala ya siasa za kimataifa haelewi hakika ya Jamhuri ya Kiislamu. Katika msimamo wake wa karibuni, Trump alidai katika kikao cha kutangaza habari ya kujiuzulu mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley kwamba: "Iran sasa ni nchi tofauti na iko siku itaketi kwenye meza ya mazungumzo na Marekani." 

Donald Trump

Donald Trump amekuwa na njozi za "kuilazimisha Iran kusalimu amri", "kubadili mienendo" na "kubadili kabisa mfumo wa utawala wa Kiislamu wa Iran". Awali aliiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na baada ya hapo akaanzisha ushirikiano mkubwa baina ya Washington, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudi Arabia dhidi ya Iran. Muungano huo umezidisha sera za propaganda chafu dhidi ya Iran kwa shabaha ya kile zinazodai ni kuitumbukiza Iran katika migogoro.

Hapana shaka kuwa, miongoni mwa malengo ya vita vya kinafsi na kiuchumi vya serikali ya Donald Trump ni kuilazimisha Iran isalimu amri na hiyo ni ndoto ambayo kamwe haitatimia. Katika uwanja huo Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran Ali Shamkhani anasema: "Iran imeishinda na kupiga mweleka Marekani katika harakati za Mapinduzi ya Kiislamu, wakati wa mashambulizi ya Saddam Hussein na katika kipindi chote cha miaka 40 ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na sasa kizazi kipya cha Iran kina fursa ya kutoa kipigo kingine kwa kizazi cha watawala washari zaidi wa Marekani wenaoongoza nchi hiyo hivi sasa."

Admeri Ali Shamkhani

Iran imekuwa ikikabiliwa na njama za aina mbalimbali za Marekani na nchi nyingine za Magharibi baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu lakini licha ya njama hizo imekuwa na machango muhimu na nafasi kubwa katika masuala ya kisiasa na kiulinzi duniani. Si hayo tu bali hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu imekuwa ikipata nguvu zaidi siku baada ya siku na kuwa na utulivu na amani zaidi kadiri siku zinavyosonga mbele.  

Nguvu mbili kuu za kubakia hai Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini ni kusimama kidete na kupambana kishujaa na adui. Katika uwanja huo naibu waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Wendy Sherman amekosoa sera za uhasama mkubwa za Donald Trump dhidi ya Iran na kusema: "Jambo ambalo Trump hajalijua ni kwamba, Iran ina utamaduni wa kusimama kidete na haitasalimu amri mbele ya vitisho."

Wendy Sherman

Iran inatekeleza sera na siasa zake kwa mujibu wa maslahi yake katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kote na haikubali kutwisha matakwa na malengo ya nchi nyingine. Suala hili linayatia hasira na hamaki madola ya kibeberu hususan Marekani ambayo siku baada ya siku inapoteza haiba na heshima yake mbele ya walimwengu. Ukweli huu ulidhihirika waziwazi katika mkutanio wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati viongozi wa nchi za dunia walipomcheka na kumkejeli Rais wa nchi hiyo, Donald Trump wakati alipokuwa akihutubia kikao hicho.