Baada ya kususiwa na China, sasa Marekani yalazimika kuipigia magoti Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49348-baada_ya_kususiwa_na_china_sasa_marekani_yalazimika_kuipigia_magoti_iran
Shirika la habari la FARS limeripoti kuwa, baada ya kupamba moto vita vya biashara baina ya China na Marekani, na hivyo China kuamua kuiadhibu Marekani kwa kususia kununua bidhaa zake za maharage ya soya, wazalishaji wa bidhaa hiyo nchini Marekani wamelazimika kukimbilia Iran ili waweze kubakia katika soko la dunia la bidhaa hiyo.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Nov 07, 2018 13:01 UTC
  • Baada ya kususiwa na China, sasa Marekani yalazimika kuipigia magoti Iran

Shirika la habari la FARS limeripoti kuwa, baada ya kupamba moto vita vya biashara baina ya China na Marekani, na hivyo China kuamua kuiadhibu Marekani kwa kususia kununua bidhaa zake za maharage ya soya, wazalishaji wa bidhaa hiyo nchini Marekani wamelazimika kukimbilia Iran ili waweze kubakia katika soko la dunia la bidhaa hiyo.

Hii ni kusema kuwa tangu mwezi Julai mwaka huu hadi hivi sasa, Marekani imeshaitumia Iran shehena 13 za maharage hayo huku shehena mbili zikiwa zimetumwa nchini Iran kutoka Marekani wiki mbili tu zilizopita.

Shirika la habari la Sputnik limelinukuu shirika la Bloomberg likisema kuwa shehena moja ya maharage hayo yenye uzito wa tani 57, wiki iliyopota ilianza safari kutoka magharibi mwa Marekani kuelekea nchini Iran na hiyo ni meli ya pili katika kpindi cha wiki moja kutoka Marekani kuelekea nchini Iran. Kwa mujibu wa Bloomberg, takwimu hizo zimepatikana kwenye mtandao wa wizara ya kilimo ya Marekani pamoja na kwenye propramu maalumu ya kufuatilia safari za meli.

Hiyo ni shehena ya 13 ya maharage hayo ya soya kutoka Marekani kuelekea nchini Iran tangu mwezi Julai mwaka huu hadi hivi sasa. Shehena 10 kati ya hizo zimetokea Mississippi na tatu zimetokea kaskazini magharibi mwa Marekani kuelekea nchini Iran.

Bandari ya mizigo cha Chabahar nchini Iran ambayo Marekani imeitoa katika orodha ya vikwazo vyake

 

Katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi hivi sasa, Marekani imeshaiuzia Iran shehena za maharage ya soya zenye uzito wa tani laki nane na 73 elfu na 420 (873,420). Marekani imelazimika kuiuzia Iran shehena zote hizo za maharage ya soya baada ya China kusususia kununua bidhaa hiyo kutoka Marekani kutokana na vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya nchi zote duniani ikiwemo China.

Kwa mujibu wa takwimu za FAOSTAT, Marekani ndiye mzalishaji mkubwa wa maharage ya soya duniani ambapo kwa mwaka inazalisha tani milioni 108 huku tani milioni 56.7 kati yake zikiwa zinasafirishwa nje ya Marekani. Nchi tano duniani ni wazalishaji wakubwa wa maharage ya soya ambapo mbali na Marekani, nchi nyingine zinazozalisha kwa wingi zaidi maharage hiyo duniani ni Brazil, Argentina, China na India. Katika upande wa pili, Iran takriban ni muingizaji mkubwa wa maharage ya soya kutoka nje ya nchi. Kwa mujibu wa takwimu wa FAOSTAT, Iran ni nchi ya tisa kwa kuagizia soya kwa wingi zaidi duniani kutoka nje ya nchi.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Novemba, vyombo vya habari vilitangaza kuwa, wakulima wengi wa Marekani wamelazimika kulima mazao mengine baada ya China kususia kununua maharage ya soya kutoka Marekani.