Mhadhiri wa Chuo Kikuu India: Marekani imeshindwa kikamilifu kuitenga Iran kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49425-mhadhiri_wa_chuo_kikuu_india_marekani_imeshindwa_kikamilifu_kuitenga_iran_kimataifa
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Bara Ulaya cha Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha New Delhi, India amesema kuwa, hatua ya Marekani ya kuziruhusu nchi kadhaa kuendelea kununua mafuta ya Iran ni ushahidi wa kushindwa kikamilifu njama za Marekani za kuitenga Iran kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 11, 2018 01:07 UTC
  • Mhadhiri wa Chuo Kikuu India: Marekani imeshindwa kikamilifu kuitenga Iran kimataifa

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Bara Ulaya cha Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha New Delhi, India amesema kuwa, hatua ya Marekani ya kuziruhusu nchi kadhaa kuendelea kununua mafuta ya Iran ni ushahidi wa kushindwa kikamilifu njama za Marekani za kuitenga Iran kimataifa.

Profesa Gulshan Sachveda, mhadhiri wa chuo kikuu hicho mashuhuri cha India amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la IRNA na huku akiisifu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa siasa zake za hekima na busara za kukabiliana na vikwazo vya Marekani amesema kuwa, matunda ya siasa hizo ni kwamba nchi nyingi duniani licha ya kuwa na uhusiano wa karibu na Marekani, zimeamua kuipinga nchi hiyo katika vikwazo vyake dhidi ya Iran.

 

Mtaalamu huyo maarufu wa masuala ya kimataifa vile vile amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mshirika muhimu na wa kuaminika wa kuidhaminia India mahitaji yake ya nishati. Ameongeza kuwa matukio ya hivi karibuni yanaonesha kuwa uchumi wa Iran una nafasi muhimu katika kuleta utulivu wa hali ya kiuchumi duniani na katika eneo zima la la magharibi mwa Asia.

Wakati huo huo Talmiz Ahmad, aliyewahi kuwa balozi wa India katika nchi za Saudi Arabia, Oman na Imarati amesema kuwa, vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran havina uhalali wowote wa kimataifa na kwamba baada ya kupita miezi sita au mwaka mmoja tu, vikwazo hivyo vitapoteza kikamilifu athari zake.