Admeri Sayyari: Mfumo wa kijeshi wa Iran ni wa kujihami na kutegemea uwezo wa kuzuia hujuma dhidi yake
(last modified Sun, 27 Jan 2019 08:01:03 GMT )
Jan 27, 2019 08:01 UTC
  • Admeri Sayyari: Mfumo wa kijeshi wa Iran ni wa kujihami na kutegemea uwezo wa kuzuia hujuma dhidi yake

Mkuu wa uratibu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, mfumo wa kijeshi wa Iran ni wa kujihami na unaotegemea uwezo wa kuzuia hujuma dhidi yake na akaongezea kwa kusema, zana zote za kijeshi na kiulinzi za vikosi vya ulinzi zinatengezwa humu humu nchini.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na kanali ya kwanza ya televisheni ya Iran, Adimeri Habibollah Sayyari amebainisha kuwa, kwa muda wote wa miaka 40 tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, zana za ulinzi za vikosi vya ulinzi vya Iran zimekuwa zikiundwa hapa nchini na ubora wake hauwezi kulinganishwa na wa kabla ya mapinduzi. Ameongeza kuwa, zana za ulinzi zinazotengezwa nchini Iran hazina tofauti kiubora na zilizo mfano wake, zinazotengezwa nje ya nchi.

Moja ya makombora yaliyoundwa nchini

Mratibu wa jeshi la Iran ameashiria pia utayari wa vikosi vya ulinzi vya Iran wa kukabiliana na kitisho cha aina yoyote ile na akasisitiza kwa kusema: Iran haina nia yoyote ya kuanzisha uchokozi kwenye mipaka na dhidi ya maslahi ya nchi zingine, lakini kama itatokea wakati ikahitajika kuonyesha nguvu na uwezo wake wa kijeshi ili kutokomeza vitisho dhidi yake, bila shaka yoyote itafanya hivyo.../

 

Tags