Pakistan yaiomba Iran ipatanishe mzozo kati yake na India
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51884-pakistan_yaiomba_iran_ipatanishe_mzozo_kati_yake_na_india
Ubalozi wa Pakistan mjini Tehran umeiomba Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran itumie ushawishi wake kusaidia utatuzi wa amani wa mzozo uliozuka baina ya nchi yake na India.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 01, 2019 23:18 UTC
  • Pakistan yaiomba Iran ipatanishe mzozo kati yake na India

Ubalozi wa Pakistan mjini Tehran umeiomba Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran itumie ushawishi wake kusaidia utatuzi wa amani wa mzozo uliozuka baina ya nchi yake na India.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, ubalozi wa Pakistan mjini Tehran umetoa taarifa rasmi na kusema kuwa, nchi hiyo muda wote imekuwa ikitahadharisha kuhusu mipango ya serikali ya India ya kutumia suala ovu la ugaidi kama kisingizio cha kujinufaisha kisiasa hasa wakati huu wa kukaribia uchaguzi mkuu nchini India.

Taarifa ya ubalozi huo wa Pakistan imeongeza kuwa, inasikitisha kuona kwamba India haikufanya hata uchunguzi au kutoa ushahidi makini wa kuthibitisha madai yake, bali unaelekeza haraka kidole cha lawama kwa Pakistan bila ya ushahidi wowote.

Kadhia ya Kashmir imekuwa ikizusha mizozo ya mara kwa mara baina ya India na Pakistan

 

Itakumbukuwa kuwa tarehe 14 mwezi ulioisha wa Februari, kundi moja la kigaidi linalojulikana kwa jina la Jeish-e Muhammad liliwashambulia wanajeshi wa India katika wilaya ya Pulwama kwenye eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India na kuua wanajeshi wasiopungua 44. Mashambulizi hayo yamezusha mzozo mpya kati ya nchi hizo mbili hasimu hasa baada ya India kutuma ndege zake na kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Pakistan katika maeneo ambayo inasema ni maficho ya magaidi hao.

Pakistan ilijibu mashambulizi hayo kwa kutungua ndege mbili za kijeshi za India zilizoingia kwenye anga yake kinyume cha sheria na kumteka rubani mmoja wa India.

India inadai kuwa imeua magaidi karibu 200 hadi 300 kwenye mashambulizi yake hayo, madai ambayo yamekanushwa na Pakistan.