Seneta wa Marekani akiri, siasa za nje za Iran ni kiboko yao..
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55606-seneta_wa_marekani_akiri_siasa_za_nje_za_iran_ni_kiboko_yao..
Seneta wa chama cha Republican cha Marekani amekiri kuwa, kuhudhuria Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika kikao cha viongozi wa G7 nchini Ufaransa bila ya kushauriwa Marekani ni ishara ya uwezo na nguvu ya siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 26, 2019 03:30 UTC
  • Lindsey Graham
    Lindsey Graham

Seneta wa chama cha Republican cha Marekani amekiri kuwa, kuhudhuria Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika kikao cha viongozi wa G7 nchini Ufaransa bila ya kushauriwa Marekani ni ishara ya uwezo na nguvu ya siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu.

Lindsey Graham amekosoa hatua ya Ufaransa ya kumwalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif katika mkutano wa viongozi wa nchi kubwa kiviwanda duniani maarufu kwa jina la G7 na kusema: Hatua hiyo ni kielelezo cha udhaifu mkubwa mbele ya Iran.

Seneta huyo mashuhuri wa Marekani amongeza kuwa: Wakati Ufaransa inapomwalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika mkutano wa G7 bila ya kushauriana na Marekani, hii ni ishara ya dharau kubwa kwa Rais Donald Trump wa Marekani. 

Jumapili ya jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif alikuwa katika mji wa Biarritz kusini mwa Ufaransa kulikofanyika mkutano wa viongozi wa G7 kwa mwaliko rasmi wa mwenzake wa nchi hiyo, Jean-Yves Le Drian, kwa shabaha ya kushauriana na maafisa wa Ulaya kuhusiana na jinsi ya kutafuta suluhisho la masuala mbalimbali. 

Zair akizungumza na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

Zarifu alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa huko Biarritz na vilevile wawakilishi wa nchi za Ujerumani na Uingereza.  

Baada ya kuondoka Ufaransa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba diplomasia ya Iran inakusudia kuwa na uhusiano jenzi na kusisitzia kuwa: Njia iliyoko mbele ya ngumu lakini inastahiki kujaribiwa.

Kabla ya safari hiyo ya Ufaransa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilitangaza kuwa, Zarif hatafanya mazungumzo ya aina yoyote na Wamarekani.