Zarif: Matumaini ya Trump ya kufanya mazungumzo na Iran, ni ndoto
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58768-zarif_matumaini_ya_trump_ya_kufanya_mazungumzo_na_iran_ni_ndoto
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter akimuhutubu Rais Donald Trump wa Marekani kwamba, juhudi za Washington za kufanyika mazungumzo ya pande mbili na Tehran ni ndoto za alinacha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2020 01:19 UTC
  • Zarif: Matumaini ya Trump ya kufanya mazungumzo na Iran, ni ndoto

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter akimuhutubu Rais Donald Trump wa Marekani kwamba, juhudi za Washington za kufanyika mazungumzo ya pande mbili na Tehran ni ndoto za alinacha.

Katika ujumbe huo Zarif amesisitiza kuwa, njia pekee ya kufanyika mazungumzo kati ya Iran na Marekani ni kupitia kundi la 5+1 na Washington kurejea katika hali ya kabla ya mwaka 2017. Ujumbe wa Mohammad Javad Zarif umekuja baada ya Rais Donald Trump kuandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter na kudai kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran eti imejiandaa kufanya mazungumzo na Marekani kwa sharti la kuondolewa vikwazo na Washington. Katika ujumbe huo Trump aliandika madai ya kuchekesha kwamba 'Washington haipo tayari kukubali sharti hilo.'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif.

Katika miezi ya hivi karibuni na viongozi wa Marekani akiwemo Trump wamenukuliwa wakitaka kufanya mazungumzo na Iran. Watawala wa Marekani mara kwa mara  wamekuwa wakizungumzia suala la kufanya mazungumzo na Iran katika hali ambayo mwaka 2018 Washington ilijiondoa kinyume cha sheria katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA ambayo yalifikiwa baada ya juhudi za miaka mingi kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1. Baada ya hatua hiyo Marekani ilianza kutekeleza tena vikwazo dhidi ya Iran.