Rais Rouhani: Umoja wa taifa la Iran umewalazimu maadui kusalimu amri
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65249-rais_rouhani_umoja_wa_taifa_la_iran_umewalazimu_maadui_kusalimu_amri
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema umoja wa taifa la Iran ni sababu kuu ambayo imepelekea maadui wa Iran kusalimu amri.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 17, 2020 12:03 UTC
  • Rais Rouhani: Umoja wa taifa la Iran umewalazimu maadui kusalimu amri

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema umoja wa taifa la Iran ni sababu kuu ambayo imepelekea maadui wa Iran kusalimu amri.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo Alhamisi katika sherehe za uzinduzi wa miundo mbinu ya miji ya Iran. Ameongeza kuwa, wote wanapaswa kusaidia katika kupatikana umoja wa taifa kwani umoja huo huleta nguvu na huwalazimisha wengine kusalimu amri mbele ya taifa.

Raouhani amesema kusimama kidete taifa la Iran katika kipindi cha miaka mitatu kutapelekea serikali ijayo ya Marekani iwaheshimu watu wa Iran, kisha irejee katika utekelezaji wa ahadi zake na hatimaye vikwazo vitasambaratishwa.

Wananchi wa Iran katika maandamano dhidi ya Marekani na Israel

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, wote wanapaswa kushirikiana katika kufanya vikwazo visiwe na athari mbaya au kupunguza athari ya vikwazo hivyo. Ameongeza kuwa, kufuatia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu ulazima wa wote kujitahidi katika kusambaratisha vikwazo, serikali itachukua hatua zinazofaa katika uga huo.

Rouhani amewaambia wananchi wa Iran kuwa, kusimama kwao kidete na muqawama ndiyo sababu kuu ambayo imepelekea adui asalimu amri mbele ya nguvu za kitaifa za Wairani.