Rais Rouhani: Uhusiano wa Iran na China ni wa kistratejia kwa Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68370-rais_rouhani_uhusiano_wa_iran_na_china_ni_wa_kistratejia_kwa_tehran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uhusiano wa taifa hili na China ni muhimu na wa kistratejia kwa Tehran.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Mar 27, 2021 21:47 UTC
  • Rais Rouhani: Uhusiano wa Iran na China ni wa kistratejia kwa Tehran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uhusiano wa taifa hili na China ni muhimu na wa kistratejia kwa Tehran.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo katika mazungumzo yake ya jana hapa mjini Tehran na Wang Yi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China na kusisitiza udharura wa kupanuliwa zaidi ushirikiano huo katika nyanja mbali mbali zikiwemo za kisiasa na kiuchumi.

Rais Rouhani ameashiria uhusiano wa kidiplomasia wa miaka 50 kati ya Iran na China na kubainisha kwamba, kuna haja ya kuharakishwa utekelezwa wa makubaliano ya pande mbili katika uga wa miradi muhimu ya miundombinu na ustawi.

Kadhalika Rais wa Iran amesifu na kupongeza misimamo ya China ya kuliunga mkono taifa hili katika majukwaa ya kimataifa yakiwemo makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, kukabiliana na misimamo ya upande mmoja na ya kupenda chokochoko ya Marekani pamoja na kulaani Beijing vikwazo vya Washington dhidi ya Tehran.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na China wakitia saini Mpango Kamili wa Ushirikiano wa Pande Zote Baina ya nchi zao

Kwa upande wake, Wang Yi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa China amesema kuwa, daima nchi yake imekuwa ikilipa umuhiimu suala la kuimarisha ushirikiano na Iran na imekuwa ikipinga siasa za kupenda kujitanua za Marekani pamoja na vikwazo vyake vya upande mmoja.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Mpango Kamili wa Ushirikiano wa Pande Zote Baina ya Iran na China ulitiwa saini jana baina ya Mawaziri wa Mashaurii ya Kigeni wa nchi hizi mbili katika sherehe maalumu iliyofanyika hapa jijini Tehran.