Ali Shamkhani: Ushirikiano wa kistratejia Mashariki unaharakisha kusambaratika Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68426-ali_shamkhani_ushirikiano_wa_kistratejia_mashariki_unaharakisha_kusambaratika_marekani
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, ushirikiano wa kistratejia wa Mashariki utaharakisha kusambaratika Marekani.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Mar 29, 2021 03:45 UTC
  • Ali Shamkhani: Ushirikiano wa kistratejia Mashariki unaharakisha kusambaratika Marekani

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, ushirikiano wa kistratejia wa Mashariki utaharakisha kusambaratika Marekani.

Ali Shamkhani amesema hayo leo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamiii wa twitter ambapo ameashiria wasiwasi ulioonyeshwa na Rais wa Marekani Joe Biden kuhusiana na kutiwa saini Mpango Kamili wa Ushirikiano wa Pande Zote Baina ya Iran na China  na kueleza kwamba, kutiwa saini hati hiyo ni sehemu ya siasa za kimuqawama ambazo ni amilifu.

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, dunia siyo ulimwengu wa Magharibi tu; na ulimwengu wa Maghariibi sio Marekani tu mkiukaji wa sheria na madola matatu ya Ulaya ambayo ni wakiukaji wa ahadi.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na China wakitiliana saini, Mpango Kamili wa Ushirikiano wa Pande Zote Baina ya nchi zao

 

Aidha Ali Shamkhani amedokeza kuwa, Joe Biden ana haki ya kuwa na wasiwasi kwani, kustawi ushirikiano wa kistratejia katika eneo la Mashariki kunaharakisha kusambaratika Marekani.

Mpango Kamili wa Ushirikiano wa Pande Zote Baina ya Iran na China ulitiwa saini Juzi Jumamaosi baina ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizi mbili katika sherehe maalumu hapa jijini Tehran.

Hati hiyo imeandaliwa na kutayarishwa katika kalibu ya mpango wa ushirikiano wa muda mrefu wa miaka 25, na ni wazi kwamba, hatua hiyo ni mwanzo wa awamu mpya katika uhusiano wa tamaduni mbili kubwa za Asia yaani China na Iran.