Rabeia: Marekani inapaswa kukomesha ukiukaji wa sheria
-
Ali Rabiei
Msemaji wa Serikali ya Iran amesema kuwa serikali ya Marekani haina njia nyingine ghairi ya kukomesha ukiukaji wake wa sheria, vikwazo vya upande mmoja na uvunjaji wa makubaliano ya kimataifa.
Ali Rabiei amewaambia waandishi habari leo mjini Tehran kwamba, hii leo kunashuhudiwa ukurasa mwingine wa kufeli na kushindwa sera za utumia mabavu za Marekani na kuhuishwa tena makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Amesema kama ilivyotarajiwa wakati wa kilele cha sera za mabavu za Donald Trump, hatimaye Marekani imekiri kuwa mashinikizo yake ya kiwango cha juu dhidi ya Iran yamefeli na hakuna njia nyingine ghairi ya kuhuishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na pande zote kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano hayo.
Amesema misimamo ya Iran kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA iko wazi na wawakilishi wa Tehran katika mazunguzmo ya Vienna watakariri tena mismamo hiyo.
Ali Rabiei amesema kwa sasa Iran haina matumaini wala haijapoteza matumaini kuhusiana na mazungumzo hayo.
Kikao cha msimu cha kamati ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kinafanyika leo mjini Vienna kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa Iran na nchi zinazounda kundi la 4+1.
Mkuu wa timu ya Iran katiika mazungumzo hayo Sayyid Abbas Araqchi, amesisitiza kuwa "kuhusu pande zote kurudi kwenye utekelezaji wa JCPOA, tutafanya mazungumzo na kundi la 4+1 tu na hatutakuwa na mazungumzo yoyote ya ana kwa ana au yasiyo ya ana kwa ana na Marekani."