Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69146-ujumbe_wa_kiongozi_muadhamu_kwa_mnasaba_wa_siku_ya_jeshi_nchini_iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi nchini Iran na kusisitiza kuwa, jeshi liko imara katika medani kwa ajili ya kutekeleza vizuri majukumu yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 17, 2021 08:09 UTC
  • Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi nchini Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi nchini Iran na kusisitiza kuwa, jeshi liko imara katika medani kwa ajili ya kutekeleza vizuri majukumu yake.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo ikiwa ni sehemu ya kuienzi Siku ya Jeshi na hamasa kubwa ya jeshi la nchi kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akimsisitizia Meja Jenerali Sayyid Abdul Rahim Mousavi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu kwamba jeshi liko imara katika medani kwa ajili ya kutekeleza vilivyo majukumu yake, hivyo hakikisheni utayari huo uko kwa kiwango cha juu kinachowezekana kwa ajili ya kutekeleza majukumu kwa namna bora kabisa.

Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amewapongeza wafanyakazi, na familia za maafisa za vikosi vya ulinzi vya Iran.

Katika upande mwingine, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa msaada wa Toman milioni 500 sarafu ya Iran kwa ajili ya kuwagomboa wafungwa wenye mahitaji maalumu katika jela za humu nchini, kwa mnasaba wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

 

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ifikapo mwezi wa Ramadhani kila mwaka, kwa hima ya kamati ya wananchi ya kuwafuatilia waliofungwa jela kwa kukosa kulipa fedha za dia na msaada kwa wafungwa wenye mahitaji maalumu, viongozi wa nchi na watu wa kujitolea mjini Tehran na katika miji mingine ya Iran huwa wanachanga pesa za kuwalipia wafungwa hao ili waende wakafunge Ramadhani na kufurahia skuukuu wakiwa na familia zao majumbani.

Mwaka huu, likiwa ni zoezi la 34 la kukusanya fedha hizo kila mwezi wa Ramadhani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa msaada wa Toman milioni 500 kwa ajili ya kuwagomboa wafungwa kwenye mahitaji maalumu katika jela za Iran.