Iran: Mbinu tunayotumia katika urutubishaji urani kwa asilimia 60, tuliipanga kabla
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69352-iran_mbinu_tunayotumia_katika_urutubishaji_urani_kwa_asilimia_60_tuliipanga_kabla
Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomoki IAEA ametoa ufafanuzi kuhusu ripoti mpya ya wakala huo akisema, mabadiliko katika mbinu ya urutibishaji wa urani ya Iran kwa asilimia 60 yamefanyika kulingana na mpango uliowekwa tangu zamani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 23, 2021 03:05 UTC
  • Iran: Mbinu tunayotumia katika urutubishaji urani kwa asilimia 60, tuliipanga kabla

Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomoki IAEA ametoa ufafanuzi kuhusu ripoti mpya ya wakala huo akisema, mabadiliko katika mbinu ya urutibishaji wa urani ya Iran kwa asilimia 60 yamefanyika kulingana na mpango uliowekwa tangu zamani.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA ulisema kuwa, urutubishaji urani wa asilimia 60 nchini Iran ni silisila inayofanyika katika kalibu ya IR6 huku silisila ya mashine za IR4 zikitengwa maalumu kwa ajili ya urutubishaji wa asilimia 20 ya urani. Sasa Mwakilishi wa Kudunu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wakala huo ametoa ufafanuzi akisema, mabadiiko hayo yalipangwa tangu zamani.

Balozi Kazem Gharibabadi ambaye pia anaiwakilisha Iran katika Taasisi za Kimataifa zenye makao yao mjini Vienna Austria aidha amesema, mabadiliko hayo ya mbinu za urutubishaji si jambo jipya na ni suala ambalo ni la kiufundi kikamilifu na kwamba Iran iliupa taarifa wakala wa IAEA kuhusu mabadiliko hayo.

Katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliamua kupandisha kiwango cha urutubishaji wa urani kwa asilimia 60 ikiwa ni katika kujibu uharibifu uliofanywa hivi karibuni na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kituo cha nyuklia za Natanz cha Iran.