Iran yataka viongozi wa kidini duniani watetee amani na uthabiti Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70246-iran_yataka_viongozi_wa_kidini_duniani_watetee_amani_na_uthabiti_palestina
Mkuu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) ametoa wito kwa viongozi wa kidini na kiutamaduni duniani kuchukua hatua za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 17, 2021 22:20 UTC
  • Iran yataka viongozi wa kidini duniani watetee amani na uthabiti Palestina

Mkuu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO) ametoa wito kwa viongozi wa kidini na kiutamaduni duniani kuchukua hatua za kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.

Katika barua yake kwa viongozi wa kidini duniani, Dkt. Abuzar Ebrahimi Torkaman amesema: "Siku hizi tunashuhudia namna ambavyo kwa mara nyingine mikono ya utawala ghasibu wa Kizayuni imejaa damu ya watoto, wanawake, na raia wengine wasio na hatia. La kushangaza ni kuwa ukatili huu unafanyika huku kukiwa na kimya cha wanaodai kutetea dmeokrasia na haki za binadamu.

Ameongeza kuwa, jinai hizo za Israel zimeumiza nyoyo za wote wanaopenda amani duniani na hivyo viongozi wa kidini duniani hawapaswa kunyamaza kimya mbele ya jinai za utawala haramu wa Israel na wanapaswa kuchukua hatua za kivitendo kuwatetea wanaodhulumiwa.

Dkt. Abuzar Ebrahimi Torkaman

Dkt. Torkman amesema inapaswa kukumbuka kuwa, amani ya kudumu Palestina, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei, itapatikana tu kwa Wapalestina wote kurejea katika ardhi zao na kisha kura ya maoni ya kuainisha hatima ya Palestina ifanyike kwa kuwajumuisha Wapalestina wote Mayahudi, Waislamu na Wakristo.