Watu wa Tehran washerehekea ushindi wa Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70434-watu_wa_tehran_washerehekea_ushindi_wa_wapalestina
Wananchi wa Tehran, mji mkuu wa Iran wameshiriki katika sherehe ya pili ya kupongeza ushindi mkubwa wa Wapalestina katika makabiliano na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 22, 2021 12:25 UTC
  • Watu wa Tehran washerehekea ushindi wa Wapalestina

Wananchi wa Tehran, mji mkuu wa Iran wameshiriki katika sherehe ya pili ya kupongeza ushindi mkubwa wa Wapalestina katika makabiliano na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza.

Sherehe hizo zimefanyika katika Medani ya Palestina katikati ya mji waTehran ambapo washiriki wamesikika wakitoa nara za  'Mauti kwa Marekani', 'Mauti kwa Israel', na  'Mauti kwa Aal Saud'.

Katika sherehe hizo washiriki wameimba wimbo wa taifa wa Palestina huku wakimunezi Shahdi Qassem Soleimani, na makamanda wengine wa muqawama waliouawa shahidi.

Ijumaa usiku pia watu wa Tehran walijumuika katika Medani ya Palestina kusherehekea ushindi wa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza

Mashambulizi ya kijinai na kichokozi ya Israel huko Ukanda wa Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hatimaye yalimalizika Ijumaa baada ya siku 12 kwa kushindwa tena kwa fedheha utawala wa Kizayuni.

Baada ya utawala wa Kizayuni kushindwa na makundi ya wanamapambano wa Palestina kwenye vita vya siku 12 vya "Saifil Quds" vilivyoisha Ijumaa usiku, televisheni ya Russia al Yaum imelinukuu gazeti la The Times of Israel likiripoti kuwa, Avigdor Lieberman, waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni ambaye pia ni mkuu wa chama cha Yisrael Beiteinu na viongozi wengine wa utawala wa Kizayuni pamoja na wabunge wa Israel, wamemlaumu vikali waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kwa kukubali kusimamisha vita kwa aibu na fedheha kubwa.