Iran: Viongozi wa Israel lazima wapandishwe kizimbani kwa jinai zao
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70564-iran_viongozi_wa_israel_lazima_wapandishwe_kizimbani_kwa_jinai_zao
Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni umefanya jinai nyingi kubwa kimataifa katika mashambulio yake ya hivi karibun dhidi ya Wapalestina hivyo viongozi wa utawala huo lazima wapandishwe kizimbani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 26, 2021 02:40 UTC
  • Iran: Viongozi wa Israel lazima wapandishwe kizimbani kwa jinai zao

Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, utawala wa Kizayuni umefanya jinai nyingi kubwa kimataifa katika mashambulio yake ya hivi karibun dhidi ya Wapalestina hivyo viongozi wa utawala huo lazima wapandishwe kizimbani.

Majid Takht-Ravanchi alisema hayo jana kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichozungumzia wajibu wa kulindwa raia katika mapigano ya silaha na kuongeza kuwa, vitendo vya kinyama na vya uangamizaji wa kizazi vilivyofanywa na Israel hivi karibuni katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina ni jinai za kivita, ni jinai dhidi ya binadamu, ni uvunjaji wa misingi yote ya kibinadamu na vimekanyaga haki zote za kimataifa za binadamu.

Majid Takht-Ravanchi

 

Amesema, kwa mara nyingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na jina hizo kutokana na uungaji mkono wa aibu wa Marekani kwa Israel. Ameelezea kusikitishwa kwake na jinsi Baraza la Usalama lilivyoshindwa hata kutoa azimio dogo tu la kuvizubaisha vyombo vya habari kuhusu msimamo wake wa kutaka kukomeshwa jinai za Wazayuni dhidi ya raia na watu wa kawaida huko Ghaza.

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa vile vile amesema, kuuliwa watu wa kawaida na kulengwa maeneo ya raia nchini Yemen kunakofanywa na wavamizi wanaoongozwa na Saudi Arabia ni mfano mwingine wa uvunjaji wa sheria za kimataifa na kusisitiza kuwa, vitendo hivyo ni jinai na inabidi vikomeshwe mara moja.

Amesema, udhaifu mkubwa unaooneshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndiyo sababu ya kuendelea kutendwa jinai kama hizo.

Israel inafanya jinai za kutisha na za kipunguani dhidi ya Wapalestina