Kamanda Salami: Zama za kupiga na kukimbia zimekwisha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70706-kamanda_salami_zama_za_kupiga_na_kukimbia_zimekwisha
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (​Sepah) ameashiria kuongezeka nguvu ya Palestina na kusisitiza kuwa zama za piga na kukimbia zimekwisha.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
May 30, 2021 03:44 UTC
  • Meja Jenerali Hussein
    Meja Jenerali Hussein

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (​Sepah) ameashiria kuongezeka nguvu ya Palestina na kusisitiza kuwa zama za piga na kukimbia zimekwisha.

Meja Jenerali Hussein Salami amesisitiza udharura wa kuzidishwa uwezo na nguvu ya Palestina na kueleza kuwa, Waisraeli wanapasa kuelewa kuwa zama zile za kupiga na kukimbia zimepita, na wananchi wa Palestina leo hii wana nguvu kubwa. Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ameongeza kuwa Palestina mpya imedhihirika. Amesema kuwa, vita vya hivi karibuni vimeiingiza Palestina yenye nguvu katika mahesabu ya utawala wa Kizayuni.  

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amebainisha kuwa Wapalestina watazidi kupata nguvu siku baada ya siku. Meja Jenerali Hussein Salami amesisitiza pia kuwa, wananchi wa Iran wataitikia maelekezo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa ajili ya kushiriki kwa wingi katika uchaguzi.  

Uchaguzi wa rais Iran kufanyika hivi karibuni 

Kamanda Salami amesema, uchaguzi si kwa ajili tu ya kumchagua rais bali kila kura inayotumbukizwa kwenye sanduku la kupigia kura ni sawa kombora linaloulenga moyo wa madola ya kiistikbari ulimwenguni; na Iran itarejea na ushindi kwa fakhari katika vita vyake vitakatifu dhidi ya ubeberu.

Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umepangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 18 mwezi huu wa Juni.