Chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa Iran kuanza kutumika rasmi wiki ijayo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70748-chanjo_ya_covid_19_iliyotengenezwa_iran_kuanza_kutumika_rasmi_wiki_ijayo
Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa hapa nchini itaanza kutumika rasmi wiki ijayo ambapo wananchi wa matabaka mbalimbali watapewa chanjo hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2021 08:54 UTC
  • Chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa Iran kuanza kutumika rasmi wiki ijayo

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa hapa nchini itaanza kutumika rasmi wiki ijayo ambapo wananchi wa matabaka mbalimbali watapewa chanjo hiyo.

Daktari Saeed Namaki amesema chanjo hiyo itatolewa kwa wale wanaotaka na hakuna atakayelazimishwa kupata chanjo hiyo ya COV-Iran Barekat

Halikadhalika amesema yeye na wafanyakazi wa Wizara ya Afya watakuwa wa kwanza kujitolea kudungwa chanjo hiyo.

Amesema hivi sasa moja kati ya chanjo bora zaidi duniani ni ile inayotegenezwa kwa ushirikiano wa Iran na Cuba na baada ya hiyo COV-Iran Barekat pia ni kati ya chanjo bora zaidi.

Jana Dkt. Hassan Jalili  mkuu wa timu ya utengenezaji chanjo hiyo ya COV-Iran katika Idara ya Utafiti ya Taasisi ya Utekelezaji wa Maagizo ya Imam Khomeini (MA) alisema tayari wameshazalisha dozi milioni moja za chanjo hiyo ambayo awamu yake ya tatu ya majaribio imekamilika. Alisema dozi hizo zitakabidhiwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kusambazwa nchini.  Amesema hivi karibuni hivi wanatarajia kuzalisha dozi milioni 18 za chanjo ya COV-Iran Barekat. 

Daktari Saeed Namaki

Hivi karibuni kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha dozi milioni 3 za COV-Iran Barekat kilizinduliwa na kwa mujibu wa makadirio wananchi wa Iran wataanza kudungwa chanjo hiyo kati kati ya mwezi Juni.

Iran iko mstari ya mbele kuunda chanjo za COVID-19 ambapo mbali na  chanjo ya  COV Iran Barakat , chanjo zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na Razi Cov Pars,  Fakhra na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.