Araqchi: Pande husika ndani ya JCPOA na Marekani zinapasa kuchukua maamuzi magumu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i70844-araqchi_pande_husika_ndani_ya_jcpoa_na_marekani_zinapasa_kuchukua_maamuzi_magumu
Mkuu wa timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia amesema kuwa pande husika ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na Wamarekani wanapasa kuchukua maamuzi magumu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2021 03:31 UTC
  • Araqchi: Pande husika ndani ya JCPOA na Marekani zinapasa kuchukua maamuzi magumu

Mkuu wa timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia amesema kuwa pande husika ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na Wamarekani wanapasa kuchukua maamuzi magumu.

Sayyid Abbas Araqchi amesema kuwa duru ijayo ya mazungumzo inaweza kuwa ya mwisho na kwamba, namna ya kurejea Marekani katika mapatano ya JCPOA na namna ya kujiridhisha Iran na baadaye kutekeleza majukumu yake ndani ya mapatano hayo, vyote hivyo vinapasa kutekelezwa kwa mujibu wa mapatano ya pande mbili na jinsi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakavyodhaminiwa maslahi yake.  

Araqchi ameeleza hayo jana usiku baada ya kumalizika duru ya tano ya mazungumzo ya Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA huko Vienna, Austria.  

Mapatano ya JCPOA yaliyopasishwa na Baraza la Usalama la UN  

Araqchi amesema, matini zinazohusu vipengee mbalimbali vya  mazungumzo tayari zimeandikwa lakini bado kuna muda hadi kufikiwa mapatano ya mwisho. Kikao cha Kamisheni ya Pamoja cha JCPOA kilifanyika jana usiku huko Vienna kikihudhuriwa na wawakilishi wa Iran na wa kundi la 4+1 linaloundwa na China, Ufaransa, Ujerumani, Russia na Uingereza. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa itatekeleza tena majukumu yake ndani ya mapatano ya JCPOA pale Marekani itakapoondoa vikwazo vyote dhidi Jamhurii ya Kiislamu na Iran kujihakikishia kwamba vikwazo hivyo vimeondolewa.