Iran yasambaratisha makundi 20 ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i7456-iran_yasambaratisha_makundi_20_ya_kigaidi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesambaratisha zaidi ya makundi 20 ya magaidi ambao walikuwa wamepanga kuripua mabomu na kutekeleza hujuma kadhaa kote nchini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2016 23:26 UTC
  • Iran yasambaratisha makundi 20 ya kigaidi

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesambaratisha zaidi ya makundi 20 ya magaidi ambao walikuwa wamepanga kuripua mabomu na kutekeleza hujuma kadhaa kote nchini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Hayo yamedokezwa na Waziri wa Usalama wa Iran Mahmoud Alavi ambaye ameongeza kuwa baadhi ya magaidi hao wameuawa na wengine kukamatwa katika oparesheni maalumu za vikosi vya usalama vya Iran. Akizungumza kabla ya hotuba za Sala ya Ijumaa Tehran, Waziri Alavi aliongeza kuwa idadi kubwa ya silaha zilikamatwa mikononi mwa magaidi hao. Halikadhalika amesema vikosi vya usalama vya Iran vimefanikiwa kugundua maeneo ambamo magaidi walikuwa wakitengengeza mabomu.

Aidha amesema Iran ina usalama wa hali ya juu katika hali ambayo nchi nyingi za Mashariki ya Kati na dunia zinakumbwa na ukosefu wa usalama.

Amebainisha kuwa pamoja na kuwepo njama za magaidi na mashirika ya kijasusi ya nchi adui, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kujidhaminia usalama na amani.