Baqeri: Wazayuni wanaweza kuwaza ndotoni tu kuishambulia kijeshi Iran
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema: Wazayuni wanaweza kuwaza ndotoni tu kuishambulia kijeshi Iran; na wakati wowote ule watakapoota ndoto hiyo hawataweza katu kuamka tena.
Shirika rasmi la habari la Iran IRNA limeripoti kuwa, Ali Baqeri, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na masuala ya kisiasa, ambaye yuko ziarani nchini Norway, ameyasema hayo mjini Oslo katika mahojiano na televisheni ya serikali ya nchi hiyo ya NRK.
Katika mahojiano hayo, Baqeri amefafanua kuhusu hatua ya karibuni iliyofikiwa katika mchakato wa mazungumzo ya kuondolewa vikwazo na kusisitiza tena kwamba shughuli za nyuklia za Iran zinafanyika kwa malengo ya amani.
Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa televisheni hiyo kuhusu jibu la Iran litakavyokuwa endapo itashambuliwa kijeshi na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Ali Baqeri amesema: Wazayuni wanaweza kuwaza ndotoni tu kuishambulia kijeshi Iran; na wakati wowote ule watakapoota ndoto hiyo hawataweza katu kuamka tena.
Katika duru ya nane ya mazungumzo ya kuondolewa vikwazo, ambayo ilisitishwa kwa muda kuanzia tarehe 11 Machi mwaka huu, suala la kupatiwa Iran mahakikisho inayotaka na kuondolewa majina ya shakhsia binafsi na wa kivyeo kwenye orodha nyekundu na majimui ya vikwazo, yangali ni masuala ambayo, Marekani, iliyo mkiukaji mkuu wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA, haijaweza hadi sasa kuchukua maamuzi ya kisiasa yanayohitajika kwa ajili ya kuyapatia ufumbuzi.../