-
Mkuu wa Idara ya Mahakama amwambia Trump: Iran ndiyo mmiliki na mtawala wa Lango la Hormuz
Aug 16, 2026 05:56Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Gholam-Hossein Mohseni-Eje’i, amezitaja kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu umiliki wa Lango Bahari la Hormuz kuwa ni "upuuzi," akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ndiyo mmiliki na mtawala halisi wa lango hilo.
-
Qalibaf: Nilisitisha mazungumzo baada ya shambulio la Israel dhidi ya Dahiyeh huko Beirut
Aug 16, 2026 03:05Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa alisitisha mazungumzo kufuatia shambulio la Israel dhidi ya eneo la Dahiyeh mjini Beirut nchini Lebanon, na kusema kuwa Iran itaushambulia utawala huo haraka iwezekanavyo.
-
Mkuu wa IRGC: Iran imelipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi duniani
Aug 15, 2026 11:00Mkuu wa Jeshi la Walinzi mwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, Iran imefanikiwa “kulipigisha magoti jeshi lenye silaha nyingi zaidi katika historia ya dunia”, kupitia operesheni za mashambulizi na ulinzi zilizotekelezwa kwa mafanikio licha ya mashambulizi makali ya adui.
-
Araghchi: Bado Hatujachukua uamuzi wowote wa kuanzisha upya mazungumzo na Marekani
Aug 15, 2026 10:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Tehran bado haijachukua uamuzi wowote wa kuanza tena mazungumzo na upande wa Marekani.
-
Iran yaitaka Ufaransa kutoa maelezo kuhusu mienendo “haramu” ya wanadiplomasia wake
Aug 15, 2026 10:57Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imeionya Ufaransa dhidi ya kuingilia mambo ya ndani ya taifa hili, ikisema kuwa Paris inapaswa kutoa maelezo kuhusu mienendo na shughuli haramu za wanadiplomasia wake.
-
Matokeo ya Kuendelea Vita: Marekani Iliyodhoofika na Iran Iliyoimarika
Aug 15, 2026 05:46Seneta mmoja wa Marekani amekiri kuwa kuendelea vita kati ya Marekani na Iran kutapelekea Marekani kudhoofika na Iran kuimarika zaidi.
-
Iran yaonyesha mabaki ya ndege za kivita za Marekani na Israel ilizozitungua +Video
Aug 15, 2026 03:54Iran imeonyesha sehemu za vifaa vilivyopatikana kutoka ndege za kivita zisizo na rubani (droni) za Marekani na Israel, pamoja na ndege ya kivita ya F-15 ambazo zilitunguliwa kwa mifumo ya ulinzi ya Iran wakati wa vita. Mifumo ya ulinzi iliyotumika kutungua ndege hizo za adui imeundwa hapa nchini.
-
Ayatullah Khatami: Uwezo wa makombora wa Iran umeidhalilisha Marekani
Aug 14, 2026 10:11Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Marekani ilitaka kuangamiza uwezo wa makombora wa Iran, lakini ilishindwa na kuufeli katika mpango wake huo.
-
Tehran: Taarifa ya Ufaransa na washirika wake wa Magharibi dhidi ya Iran ni propaganda za kinafiki za kupotosha ukweli
Aug 14, 2026 10:09Kaimu Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hatua ya Ufaransa na baadhi ya nchi za Magharibi ya kutoa taarifa ya pamoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kisingizio cha masuala ya haki za binadamu na kusema kuwa hatua hiyo ni mfano wa wazi wa unafiki wa kupotosha uukweli wa mambo.
-
Iran: Hakuna chombo kinachoweza kupita salama Hormuz bila idhini
Aug 14, 2026 03:31Msemaji wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ijulikanayo kama Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya amekanusha madai ya Marekani kwamba meli zinaendelea kupita kwa hali ya kawaida katika Lango Bahari la Hormuz, akisema hakuna chombo kinachoweza kuvuka kwa usalama njia hiyo ya kimkakati bila idhini na uangalizi wa Iran.