-
Wanamgambo wa RSF wadai kutwaa makao makuu ya jeshi la Sudan katika mji wa al Fasher
Oct 26, 2025 23:25Mapigano yalipamba moto jana Jumapili katika mji uliozingirwa wa al Fasher huko Sudan katika jimbo la Darfur Kaskazini, huku kundi la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) likidai kuiteka kambi ya jeshi la Sudan (SAF).
-
MSF: Israel inaendelea kutumia misaada ya Gaza kama silaha ya vita
Oct 26, 2025 23:13Afisa mkuu wa shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) anasema utawala wa Israel unaendelea kutumia misaada ya kibinadamu huko Gaza kama silaha ya vita dhidi ya Wapalestina.
-
PKK yatangaza kuondoka Uturuki kama sehemu ya mchakato wa kuweka chini silaha
Oct 26, 2025 23:09Kundi la wanamgambo wa Kikurdi la PKK limetangaza rasmi uamuzi wake wa kuondoa wapiganaji wake wote nchini Uturuki kuelekea kaskazini mwa Iraq, kama sehemu ya mchakato wa kuweka chini silaha.
-
Qalibaf: Barua ya Iran-Russia-China kwa UN inaonesha mshikamano wa kimkakati dhidi ya vikwazo
Oct 26, 2025 08:31Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, barua ya pamoja ya hivi karibuni iliyotumwa na Iran, Russia na China kwa Umoja wa Mataifa kupinga jaribio la nchi za Ulaya la kurejesha vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu inaonesha "mshikamano wa kimkakati" uliopo baina ya mataifa hayo matatu yenye nguvu.
-
Russia yazindua kombora jipya linalotumia fueli ya nyuklia
Oct 26, 2025 08:31Rais Vladimir Putin wa Russia amezindua kombora jipya linalotumia fueli na mafuta ya nyuklia linaloitwa Burevestnik wakati wa kukagua kituo cha mstari wa mbele cha vita vinavyoendelea kati ya Russia na Ukraine
-
Zaidi ya mashtaka 1,500 yamefunguliwa Morocco baada ya maandamano ya Gen Z
Oct 26, 2025 08:30Asasi isiyo ya kiserikali ya Morocco imesema kwamba zaidi ya watu 1,500 walioshiriki katika maandamano yaliyoenea katika kona zote za Morocco wakidai huduma bora ya afya, elimu na kukomeshwa ufisadi, wamefunguliwa mashtaka na serikali. Maandamano hayo yalidumu kwa mwezi mzima.
-
AU yahimiza kuchukuliwa hatua madhubuti za kudhamini chakula Afrika
Oct 26, 2025 08:30Kamishna wa Kilimo, Maendeleo Vijijini, Uchumi wa Bluu na Mazingira Endelevu wa Umoja wa Afrika (AU), Moses Vilakati ametaka kuchukuliwe juhudi zaidi na zilizoratibiwa vyema kwenye bara zima la Afrika ili kushughulikia changamoto kubwa za usalama wa chakula barani humo.
-
Zimbabwe yatoa mwito wa kuondolewa vikwazo vya Magharibi bila ya masharti
Oct 26, 2025 08:29Jana Zimbabwe ilifanya maadhimisho ya Siku ya Kikanda ya Kupinga Vikwazo huko Harare, mji mkuu wa nchi hiyo. Wananchi wa Zimbwe wametaka kuondolewa vikwazo vya nchi za Magharibi bila ya masharti na kuruhusiwa taifa lao kufanikisha malengo yake ya ustawi wa kiuchumi.
-
Ufaransa yatangaza kuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine
Oct 26, 2025 06:49Pars Today- Mkuu wa Komandi Kuu ya Jeshi la Ufaransa ametangaza kwamba ikiwa Russia na Ukraine zitafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, Paris itakuwa tayari kutuma wanajeshi nchini Ukraine kama sehemu ya kutoa dhamana za usalama kutoka kwa nchi za Magharibi.
-
Hamas: Israel imeshindwa kufikia malengo yake kupitia mauaji ya kimbari
Oct 26, 2025 04:37Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Ukombozi wa Palestina, Hamas, limesisitiza kuwa utawala wa Israel umeshindwa kufanikisha malengo yake kupitia vita vya zaidi ya miaka miwili vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.