-
Iran yamuonya mkuu wa IAEA: Vitisho vilivyofeli havitaleta isipokuwa kusindwa kwingine
Oct 24, 2025 00:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amemuonya mkuu wa shirika la nyuklia la Umoja wa Mataifa, Rafael Grossi, dhidi ya kutoa "vitisho vilivyoshindwa" dhidi ya Tehran, akisema matamshi kama hayo hayataleta "isipokuwa kushindwa kwingine."
-
WFP: Kiwango cha chakula kinachoingizwa Gaza ni kidogo mno
Oct 24, 2025 00:49Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) limetangaza kuwa, kiwango cha chakula kinachoingia Gaza bado kiko chini sana ya lengo la tani 2,000 kwa siku, likitoa wito kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kufungua vituo zaidi vya mipakani.
-
Mashabiki wa Galatasaray wapamba majukwaa kwa bendera ya Palestina, wataka kukomeshwa mauaji ya kimbari Gaza
Oct 24, 2025 00:49Mashabiki wa Galatasaray wa Uturuki wakitangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina walipamba majukwaa ya uwanja wa Rams Park kwa bendera ya Palestina na kutoa wito wa kukomeshwa mauaji ya kimbari huko Gaza.
-
Matokeo ya uchaguzi wa rais wa Cameroon kutangazwa Jumatatu
Oct 23, 2025 23:25Baraza la Katiba la Cameroon linasema kuwa litatangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais siku ya Jumatatu tarehe 27 Oktoba, saa 11 asubuhi kwa saa za huko.
-
Mahdieh Esfandiari Muirani mtetezi wa Palestina aachiliwa huru
Oct 23, 2025 23:24Mahdieh Esfandiari, mwanaharakati wa Iran anayewaunga mkono watu wa Palestina, ameachiliwa kwa masharti kutoka katika jela ya Ufaransa baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya miezi saba.
-
Ni mambo gani yameifanya Israel itengwe kisiasa na kijamii kiasi hiki?
Oct 23, 2025 23:02Israel inakabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa katika historia yake. Yair Lapid, kiongozi wa upinzani wa utawala wa Kizayuni, alikiri hivi karibuni katika kikao cha kamati moja ya Knesset kwamba Israel hivi sasa iko katika mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa katika historia yake.
-
Hamas: Miswada haramu ya unyakuzi wa Ukingo wa Magharibi inafichua sura mbaya ya ukoloni wa Israel
Oct 23, 2025 07:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imelaani pendekezo la awali la Bunge la Israel (Knesset) la kunyakua eneo la Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, na kusema kuwa hatua hiyo inaakisi sura mbaya ya ukoloni wa utawala wa Tel Aviv katika ardhi ya Palestina.
-
Waziri wa Usalama wa Taifa: Iran haina imani kuhusu kulindwa maslahi ya taifa kupitia mazungumzo na Marekani
Oct 23, 2025 07:47Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu haina imani kabisa kuhusu kulindwa maslahi ya nchi hii kupitia kufanya mazungumzo na Marekani.
-
Je, kujenga vinu vya nyuklia kutaiwezesha Afrika au kutaimarisha utegemezi wa kigeni?
Oct 23, 2025 07:44Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed mwezi uliopita alitangaza mipango ya kujenga vinu vya kwanza vya nyuklia nchini humo na hivyo kuashiria hamu kubwa ya bara la Afrika ya kumiliki nishati ya atomiki. Nchi za bara la Afrika zinahitaji kukidhi mahitaji ya nishati yanayoongezeka kila siku na kupunguza utegemezi wa nishati ya kisukuku.
-
Mahakama ya ICJ: Israel inapasa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza
Oct 23, 2025 07:40Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeitaka Israel ijiepushe kutumia sheria zake za upande mmoja maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na kuukosoa utawala huo ghasibu kwa kuzuia kufikishwa misaada ya kibinadamu katika eneo lililoharibiwa na vita la Gaza.